Serikali itunge sheria kudhibiti Mapromota wahuni katika mchezo wa ngumi, vinginevyo mchezo huo utaonekana wa kihuni

Serikali itunge sheria kudhibiti Mapromota wahuni katika mchezo wa ngumi, vinginevyo mchezo huo utaonekana wa kihuni

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Nimemsikiliza mdigo mwenzangu, sisi watu wa Tanga sio malofa, kwanza ngumi ndio fani zetu, kuna wakati tulikuwa tunacheza mechi za ngumi za uswahili maeneo ya Makorola, yaani mabondia wa Donge au usagara wanapambana na mabondia wa makorola, tunakutana eneo tunalopanga kila mmoja anachagua wake zinapigwa kavu kavu.

Tanga ndio anakotokea Magoma Shaaban, Bakary Mambeya nk, sisi ngumi ni kama mpira wa miguu vile.Mie mwenyewe ukiniingia vibaya nakuchafua uso dakika 2 t, ndio maana wanaonitukana humu nawaangalia t.

Mwakinyo kakataa ulofa, mapromota wetu wahuni, sio professional, wanataka kutajirika kupitia mabondia, kwa mfano Mwakinyo kasema Leo hapigani lkn watu wanafosi kusema Mwakinyo amekubali na mgogoro umeisha wakati Mwakinyo amegoma kweupeeeee.

Acheni wizi, Mwakinyo alitoa hela zake ili mradi sisi mashabiki zake tufurahi Leo lakini mnamchanganyia mfaili, kwanini mumtafutie mapromota aliokataa kufanya nao kazi?

Acheni kuharibu brand za watu, serikali iiingilie kati mapromota feki wachukuliwe hatua, serikali itengeze sheria promota wa ngumi awe na vigezo na leseni ili kuwaondoa wahuni kwenye mchezo huo mgumu sana.
 
Toka kiongozi wa shirikisho la ngumi apewe kipaza sauti ikulu aongee changamoto zinawakabilia mabondia, akaishia kushukuru kwa wali aliyokula Ikulu.

Mwakinyo naye akaibuka na kumwita ni mpuuzi kwenye interview kwa kushinda kuwasemea changamoto zao na kusifia wali wa ikulu.

Naona kama huyo jamaa na genge lake wanafanya mambo kumkomoa sana, kuna vitu anavyofanyiwa si vya haki huyu jamaa.
 
Nami nimemsikiliza mwakinyo naona yupo sahihi kabisa, hivi bondia gani bongo anaweza kulipa dollar 4000 ili kutatua matatizo yaliopo ya promota ilimladi tu apigane? katumia uungwana sana ila wenye chuki tu ndo wataona kazingua
 
Umesikiliza upande wa pili?
 
Nami nimemsikiliza mwakinyo naona yupo sahihi kabisa, hivi bondia gani bongo anaweza kulipa dollar 4000 ili kutatua matatizo yaliopo ya promota ilimladi tu apigane? katumia uungwana sana ila wenye chuki tu ndo wataona kazingua
Ngumi/ masumbwi/ ndondi ni mchezo unaokuathiri mchezaji moja kwa moja. Ukipigwa, unapigwa usoni kwako, sio kwa mwingine
 
Mie nilipomsikiliza kwa kinywa chake mwakinyo kuwa walikuwa na Mkataba wa Maneno ( porojo ) baine yao nimeshindwa kabisa kuelewa inakuaje Bondia wa Kimataifa kushindwa kujua mambo ya msingi

Ila ndio tulivyo wa bongo

Mie kuna Jamaa ninaheshimiana alitaka nimkopeshe kapesa kadogo tu nikamshauri aje tuandikishiane kuonesha nimemkopesha na atanirudishia lini tena Mkopo usio na riba …akanihesabu nina roho mbaya na akakata hadi mawasiliano eti kisa simuamini

nilichagua upande huo kwa usalama wa muamala wangu

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom