Saint_Maxi
Member
- Jan 11, 2021
- 25
- 16
Ukara wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza kuna shirika la umeme (JUMEME) linahusika na huduma ya usambazaji wa umeme wa nguvu ya jua ila kero ipo kwenye bei.
Bei ni Elfu mbili 2000/= kwa kila unit, na namna ya huduma ya kila mteja katika matengenezo yao, kwasababu mita ina tatizo ukimtafuta fundi wao anakupost kwa shushushu wao hapa Malelema kisiwani Ukara ili aje aangalie na hana taaluma yoyote inayohusu umeme.
Pili, ikishindikana fundi wa kampuni anatumia huyo shushushu kumshawishi mteja atoe pesa ya usafiri na matengezo ya kifaa chao nje na mkataba wa kampuni na mteja.
Hii imekuwa kero ni bora serikali iingilie kati na kuweka mambo sawa au kampuni kongwe na umeme nchini isogeze umeme wao japo ni wa mgao ila ni nafuu kulinganisha na hawa wanaosambaza umeme kwa nguvu ya jua na bado ni ghari.