BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mimi natokea Mkoa wa Tabora, Wilaya ya Kaliua, Kata ya Kashishi, kero yetu hapa ni barabara ya kutoka Kahama Mkoani Shinyanga kwenda Kaliua Mjini (Tabora) kupita Unlyankuru, Mwamnange na Kashishi.
Kwani barabara hii ni muhimu kwetu sisi Wakulima tunaitumia kusafirisha mazao kupeleka kwenye soko la Kahama ila hii barabara ni mbovu, magari hukwama njiani mara kwa mara na kusababisha hasara kwa Wakulima, Wamiliki wa magari na watumiaji wengine mbalimbali.
Nyakati za mvua hali ndio inazidi kuwa mbaya, tunaomba Serikali kupitia wizara husika itujengee lami, kwani ni barabara muhimu kwa uchumi wa Wilaya yetu ya Kaliua.