Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara za mitandaoni ili kuziboresha na kupanua wigo wa walipa kodi pamoja na kuboresha huduma za posta

Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara za mitandaoni ili kuziboresha na kupanua wigo wa walipa kodi pamoja na kuboresha huduma za posta

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
1,492
Reaction score
2,361
Napenda kuishauri serikali iunde chombo cha kusimamia biashara za mtandaoni ili kuziboresha na kupanua wigo wa walipa kodi.

Binafsi mimi ni mfanyabiashara wa online, kwa uzoefu wangu kufanya biashara online naweza kusema ni sehemu nzuri ya kufanyia biashara na inafanya iwe rahisi sana kwa mnunuaji kuwasiliana na muuzaji ila tunakabiriwa na changamoto nyingi sana.

Naamini serikali ikiunda chombo cha kuisimamia na huduma za posta zikaboreshwa wajasiriamali wengi wa online tutafanikiwa sana.

Kwanini chombo cha kuisimamia? Chombo hicho kije na ubunifu wa kusajiri wote wanaofanya biashara online kwa ada ndogo na kuwapa namba za utambulisho ili kupunguza wimbi la matapeli. Pia iwe ni rahisi kwa mnunuzi kutoa malalamiko yake pale panapotokea utapeli. Tunaweza kujifunza kwa aliexpress na amazon, wao wana mifumo ya kusimamia kiasi ambacho hakuna anayeweza fanya utapeli huko. Hili litaongeza kuaminiana hivyo kuongeza mzunguko wa online business.

Kwanini tuboreshe huduma za posta? Kutuma mizigo kwa mabasi kuna changamoto nyingi sana. Tukiboresha posta yetu naamini mizigo mingi itafika kwa mlengwa kwa wakati sahihi na kwa gharama ndogo.

Mwisho wa siku serikali itakusanya mapato mengi sana, kikubwa izibgatie tozo zisiwe kubwa za kutuua.
 
SIJAWAHI ONA PANYA ANAPELEKA PROPOSAL YA YA KUUNDA MTEGO WA PANYA KWA PANYA WENZIE
 
Itakuwa EWURA nyingine
Inapandishwa bei ya bidhaa halafu uchambuzi unafuata wakati watu tayar wanalipa
 
Back
Top Bottom