Likunguniz
New Member
- Aug 20, 2023
- 1
- 2
Nawasalimia ndugu na jamaa zangu,
Ama baada ya salamu, naomba kuelekekeza mawazo yetu kwenye mada hii.
Wizara ya Maliasili na Utalii, Pamoja na majukumu yake mapana, ina Taasisi na mashirika ya umma yaliyo chini yake. Miongoni mwa Taasisi na mashirika hayo ni:
1. Hifadhi za Taifa (TANAPA)
2. Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA)
3. Mamlaka ya HIfadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA)
4. Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)
5. Bodi ya Utalii (TTB)
6. Makumbusho ya Taifa Tanzania (NMT)
Hadi kufikia Mwaka huu, kuna jumla ya Hifadhi za Taifa 22 zinazosimaiwa na TANAPA, Mapori ya Akiba 27 na Mapori Tengefu 27 ambayo yanasimamiwa na TAWA na Eneo la Ngorongoro NCAA. Maeneo haya yaliyotengwa kwa ajili ya Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu ni Kilometa za Mraba 307,800 sawa na asilimia 32.5 ya eneo lote la nchi yetu.
Mashirika haya matatu (TANAPA, TAWA na NCAA) kimsingi wanatekeleza majukumu yanayoshabihiana licha ya kila Taasisi kuwa na sheria yake iliyoanzisha, pia kuna baadhi ya sheria ambazo zinatekelezwa kwa Pamoja.
Mashirika haya yanafanya ushindani usio na afya kwa serikali, kwa mfano:
1. Kila Taasisi ina madaraja yake ya mishahara, NCAA na TANAPA yanalipa mishahara na marupurupu mazuri, huku TAWA na TFS wakiwa na maslahi hafifu.
2. TAWA inadidimizwa kwani kila inapojaribu kutengeneza mapori yanayoweza kuzalisha pesa kwa utalii au uwindaji, mapori hayo yanabadilishwa kuwa hifadhi za Taifa na wao kuachwa bila kitu.
3. Shirika kama NCAA linapotengeneza friction za ndani mara nyingi limeonekana kuwahamisha watumishi wake kwenda TAWA kwenye maslahi madogo kama vile ishara ya adhabu.
Mimi napendekeza na namshauri kwa unyenyekevu kabisa Mh. Rais:
1. Haya Mashirika yote yaunganishwe na yawe na Kamishna mmoja tu, Muundo mmoja, Bodi ya wakurugenzi moja, na Budget moja tu.
2. Shirika moja litakoundwa liitwe Mamlaka ya Wanyamapori na Misitu Tanzania. Ndani yake itakuwa na Kurugenzi ya Utalii, Uhifadhi, Malikale n.k
3. Hii itasaidia kustabilize hata wizara yenyewe (Hii ni wizara inayoongoza kwa kubadili mawaziri kila leo) na sababu ni misuguano ya hizi Taasisi tatu.
Kuungwa kwao kutaleta ufanisi na mgawanyo sawa wa maslahi na majukumu ya Uhifadhi wa rasilimali za nchi yetu.