Serikali Iunge Mkono Juhudi za Wananchi Ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Tanganyika

Serikali Iunge Mkono Juhudi za Wananchi Ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Tanganyika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE MARTHA MARIKI - SERIKALI IUNGE MKONO JUHUDI ZA WANANCHI UJENZI WA KITUO CHA POLISI KATIKA WILAYA YA TANGANYIKA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi, Mhe. Martha Festo Mariki katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ameuliza mpango wa Serikali kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi katika Wilaya ya Tanganyika.

"Wilaya ya Tanganyika hatuna kabisa kituo cha polisi, lakini wananchi wa Wilaya ya Tanganyika wameonyesha juhudi kwa kuanzisha ujenzi wa kituo cha Polisi kwa kujenga Msingi" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Je, ni lini Serikali itaunga juhudi za wananchi kwa kutupatia fedha ili tuweze kukamilisha ujenzi wa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Tanganyika"? - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Nimuahidi Mhe. Martha Festo Mariki kwamba tunatambua umuhimu wa kuwa na kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya na Vituo vingine vya polisi kwenye Tarafa katika Wilaya ya Tanganyika." - Mhe. Jumanne Sagini, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

"Kwenye bajeti ijayo ya mwaka 2023-2024 tutaona uwezekano wa kuwachangia ili waweze kujenga Kituo hicho (Kituo cha polisi katika Wilaya ya Tanganyika). Tumuombe Mwenyezi Mungu liwezekane liweze kutekelezwa" - Mhe. Jumanne Sagini, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
 

Attachments

  • IMG_5199we.jpg
    IMG_5199we.jpg
    209.7 KB · Views: 6
  • maxresdefaultqwer.jpg
    maxresdefaultqwer.jpg
    130.9 KB · Views: 5
Back
Top Bottom