Serikali iwasaidie wakulima wadogo

Serikali iwasaidie wakulima wadogo

ItsMi

Member
Joined
Sep 13, 2021
Posts
66
Reaction score
31
Serikali iwasaidie wakulima wadogo wadogo katika kuwawezesha kunufaika na kilimo kilicho bora.
Na tunajua kwamba Kilimo ni uti wa mgongo kwa taifa ambapo lishe yote ya wananchi inategemea juhudi au jitahada za mkulima katika maswala mazima ya kupanda na kupalilia mazao na hatimaye kufanya mavuno ya mazao hayo na kuyapeleka sokoni kwa ajili ya mauzo ambapo watu watakwenda kununua bidhaa hizo.

Lakini hawa wakulima wadogo ndio ambao tunawategemea kwa baadae kuja Kuwa wakulima wakubwa kwa hapo baadae ambapo kwa sasa wanahitaji wapate msaada wa kiserikali na wadau wengine wa kilimo katika kuwapa elimu inayohusu maswala mbalimbali ikiwemo Kuwapa elimu inayohusu kilimo cha kisasa ili kwamba waweze kufanya uzalishaji mkubwa wa mazao pia kujua aina za wadudu na madawa ya kuyatumia katika kilimo hicho wawapo shambani.

Pia kuwajuza kuhusu mbegu gani ni bora kwa uzalishaji wa mazao hayo ili kuongeza uzarishaji na kuendana na soko la bidhaa husika na katika kuingia katika ushindani wa bidhaa bora kwa kuzingatia mbegu mbolea na madawa pamoja na uangalizi wa karibu

Na hata kufikia hivi sasa wanayodhamira ya kufika mbali japokuwa wanakutana na vikwazo mbalimbali ikiwemo magonjwa yanayoshambulia mazao ambapo hushambuliwa mno na wadudu mbalimbali hali inayopelekea kudhoofisha uzalishaji wa zao husika.

Pia changamoto yao nyingine ni kwenye. Ongezeko la bei pembejeo za kilimo zinazobadilika kila mwaka

Pia wanakumbwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo hawajui ni namna gani ya kuweza kukabiliana nazo.

Bei ya mazao isiyoeleweka Kwa maana pindi wanapotaka kuipeleka bidhaa hiyo sokoni wanakutana na bei zinazowakandamiza wakulima kwa ujumla jambo linalopekea kuwakatisha tamaa wakulima walio wengi

Pia ukosefu wa ujuzi wenye kutosheleza wao kukabiliana na hizo changamoto mbalimbali ni kikwazo kikubwa kwa upande wao.

Hivyo tunaiomba serikali iwape ushirikiano mkubwa ili wafanikiwe katika kilimo na waweze kufika mbali katika kuinua uchumi wa nchi.

Asante.
 
Habari za leo. Karibu Jf
Umesema vyema.
Ili serikali iweze kuwasaidia wakulima hawa wadogo wadogo ni muhimu sana waungane na kuwa na umoja wao.

Kwa uzoefu wangu ni rahisi serikali kuwasaidia wakulima wakubwa. Kwa kuwa tayari hao wanatambulika.

Wakulima wadogo wadogo wakijiunga wanaweza kusaidiwa na serikali na taasisi nyinginezo maana inakuwa rahisi kupewa mafunzo, kununua pembejeo kwa ujumla na kupunguza bei. Kupata zana za kilimo kwa bei nzuri. Mf matrekta, ambayo yataweza kuwasaidia. Kutafuta masoko kwa pamoja na faida nyingine nyingi.

Faida nyingine ni kukutana na wote wenye changamoto za iana moja na kuzitafutia ufumbuzi. Maana wataweza kuchangia mawazo na kupata namna ya kujikwamua.
 
Jukumu la serikali kuwasaidia wakulima wadogo ni wajibu wao ndio maana kuna bwana shamba wa serikali ambaye kazi yake ni kuelekeza na kufundisha wakulima
Tatizo wakulima ni wengi mno na bwana shamba ni wachache sana.
 
Wakulima ni rahisi kujifunza kwa wakulima wenzao au kupitia shamba darasa.
 
Back
Top Bottom