SoC04 Serikali iwaunganishie wananchi umeme bure, wakatwe kwenye luku. TASAF iweke utaratibu wa kuzilipia kaya masikini

Tanzania Tuitakayo competition threads

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,011
Reaction score
1,681
Tanzania tuitakayo baada ya miaka mitatu

SERIKALI IWAUNGANISHIE WANANCHI UMEME BURE, WAKATWE KWENYE LUKU, KAYA MASIKINI TASAF IWEKE UTARATIBU WA KUWALIPIA

Gharama za kuunganishiwa Umeme ni Kubwa sana kwa mujibu wa Tovuti rasmi ya Tanesco imeweka gharama za kuunganishiwa umeme ni kama ifuatavyo Uunganisho wa Umeme Vijijini na mijini kwa umbali usiozidi Mita 30 na miundombinu ya karibu iliyopo ni TZS 27,000.

Uunganisho wa umeme mijini kwa umbali usiozidi Mita 30 na miundombinu ya karibu iliyopo ni TZS 320,960.00.

Wateja wa Vijijini wanaohitaji umeme ambapo Miundombinu iliyopo ya TANESCO ipo ndani ya mita 60 ni TZS 337,740.00

Wateja wa Mijini wanaohitaji umeme ambapo Miundombinu iliyopo TANESCO ipo ndani ya mita 60 ni TZS 515,618.00

Wateja wa Vijijini wanaohitaji umeme ambapo Miundombinu iliyopo ya TANESCO ipo ndani ya mita 90 ni TZS 454,654.00

Wateja wa Mjini wanaohitaji Umeme ambapo Miundombinu iliyopo TANESCO ipo ndani ya mita 90 ni TZS 696,670.00

Wananchi wengi wa Tanzania hawana uwezo wa Kumudu Gharama za Kujiunganishia umeme, Hususani ameneo ya Vijijini ambao hawajapitiwa na Mradi wa Umeme vijijini kupitia kwa WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)

Janury 17 2024 Kaimu Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Thomas Mmbaga alisema kuanzia vijiji Vijiji 758 kati ya Vijiji 12,315 vilivyopo nchi nzima;havijafikiwa na Mradi huo.

kwa mujibu wa Matokeo ya Utafiti wa Athari yaUpatikanaji wa Nishati Endelevu (IASES) 2021/22, yanaonesha kuwa takriban asilimia 46 yaka ya zimeunganishwa na umeme kwa Tanzania Bara.

Asilimia ya kaya zilizounganishwa na umeme ni kubwa zaidi katika maeneo ya mijinii kilinganishwa na maeneo ya vijijini.

Karibu kaya tisa kati ya kumi kwa mkoa wa Dares Salaam (87 asilimia) na kaya saba kati ya kumi katika maeneo mengine ya mijini (70asilimia) zimeunganishwa na umeme. Kwa upande mwingine, takriban kaya nne katiya kumi (36 asilimia) zimeunganishwa na umeme katika

Kwa mujibu wa Takwmu hizi zaidi ya kaya 54% hazijaunganishwa na huduma Hii muhimu ya Umeme.

Wananchi wengi wana hitaji umeme, kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yale ya kibiashara lakini wanashindwa Kumudu gharama za kuunganishiwa Umeme.

Serikali inaweza Kuweka utaratibu mzuri unaofaa na usioumiza kwa kuwaunganishia wateja wote wanaohitaji Umeme kisha iweke utaratibu mzuri wa wateja wao kulipia gharama hizo kila Mwisho wa mwezi kwa kukata Moja moja Pindi anaponunua LUKU.

Kwa mapendekezo ninayopendekeza Kwa mjini wakatwe Angalau elfu kumi kila mwezi Kwa muda wa Miaka mitatu na Kijini elfu tano kila mwezi kwa muda wa Miaka mitatu au Pia kwa jinsi ambavyo Serikali itaona inafaa.

FAIDA ZA ZAKE NI

Hii itasaidia TANESCO kuwa na wateja wengi wanaotumia Umeme na hivyo Moja moja itaongeza mapato ya shirika hilo kwa sababu wateja watakuwa wakinunua umeme kwa wingi

Wananchi Kuongeza kipato kwa Kutumia fursa zinazotokana na Upatikanaji wa umeme.

Kufungua Fursa nyingi za kiuchumi Katika maeneo ya Vijijini

Faida nyingine ni Kwamba tunatambua Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya changamoto kuu zinazoisumbua dunia kwa sasa.

Ili kukabiliana na athari mabadiliko hayo ikiwemo ukame, mafuriko na ongezeko la joto, watalaam wa mazingira wanapendekeza matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia na mwanga hivyo upatikanaji wa umeme utapunguza matumizi ya Kuni na mkaa ,Bila kusahau pia itapunguza kwa kiwango kikubwa uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo.

Lakini pia itawafanya wananchi wanufaike moja kwa moja na uwekezaji unaofanywa na serikali katika utekelezaji wa miradi Mikubwa ya kimkakati iikiwemo wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) Unaotarajia kuzalisha zaidi ya Megawati 2115 za Umeme.

KWA WALE WANANCHI AMBAO HAWANA UWEZO KABISA AMBAO NI WANUFAIKA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI, AMBAO UNATOA RUZUKU KWA KAYA MASKIN;

Serikali inaweza hawa badala ya kuwapa fedha taslimu ikaweka utaratibu mzuri pia utakaowawezesha Kulipia gharama hizo kupitia uwezeshaji wa kifedha wanaotoa kila mwezi katika kaya Hizo ili kuboresha maisha yao.

Mpango huu uende sambamba na Kutoa Elimu kwa wananchi Juu ya Utunzanji wa Mazingira na ujenzi wa nyumba za kisasa za Kuishi pamoja na matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupata mwanga na Kupika.

Pia serikali inaweza kuangalia namna ya kushirikisha wadau wengine wa maendeleo Katika kutekeleza Hili suala ambalo litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi

Kwa kuanzia serikali kupitia wizara ya nishati inaweza kulichukua na kujadili namna utekelezaji wake unavyoweza kufanyika na mwaka Ujao wa fedha 2024/2025 serikali ikaja na mkakakati madhubuti

Mwisho wazo hili likuchukuliwa kwa uzito na kufanyiwa kazi kwa kipindi cha Miaka Mitano ijayo kuanzia 2025-2030 wananchi wote watakuwa wameunganishiwa huduma ya Umeme na KUongeza pia idaidi ya wananchi wanaotumia nishati safi Kupikia, lakini pia itaboresha makazi hasa maeneo ya vijijini.

MWANDISHI NI YOHANE GERVAS MASSAWE
EMAIL GERVASYOHANE@GMAIL.COM
TABATA DAR ES SALAAM
 
Upvote 70
Madhara ya Muungano ni pamoja na hili la umeme.Tulipokuwa tunaongozwa na mtanganyika tulilipia 27000 lakini tulipotawaliwa na mgeni kutoka Zanzibar bei imepanda Hadi 321000 ndani ya mita 15.
 
hahaha matobo ya Muungano
 
Nimegundua kuwa Utaratibu wa Tauzo unaofanywa na Chama Chama Mapinduzi ndio unaotuletea hali mbaya ya kimaendeleo Kwa serikali na Kwa wananchi.

Viongozi wengi wanaoteuliwa hawajui jata jukumu lao la kuwaletea wananchi maendeleo . Wengi wanawaza uchaguzi na kupiga Hela basi.

Kuna Mkuu wa mkoa wa Tanga alifika kwenye Eneo la mradi mkubwa wa Kilimo Cha Umwagiliaji . Ni mradi wa Serikali uliowekwa Kwa ajili ya maendeleo ya Wakulima wa vijiji ziaidi ya 30 kwenye Bonde Moja kubwa sana kuanzia Bwiko mpaka Msambisi.
Mradi Huo ulikua unafanywa na wachina Kwa kujenga Bwawa kubwa la maji maeneo ya Manga. Na Kisha kuweka miundombinu Bora Kwa ajili ya kumwagilia mashamba ya wananchi. Cha ajabu wakajitokeza wazee wenye umri mkubwa wasiojua umuhimu wa mradi Huo na jinsi utakavyotoa ajira Kwa vijana wengi , wakawashawishi watu Kwa kuangalia maslahi binafsi na kupotosha kuwa maji yatafurika mpaka kwenye Nyumba zao na watu watazama kwenye maji hivyo Huo mradi haufai usitishwe.
Jambo la kusikitisha zaidi Mkuu wa mkoa akawaunga mkono na kusimamisha mradi Huo mkubwa ambao ungeleta tija na ajira Kwa vijana wengi Kwa Karne zijazo.

Yaani badala ya mkuu wa mkoa kuwaelimisha watu juu ya umuhimu wa Kilimo Cha Umwagiliaji katika Karne hii yeye anaungana na wajinga kuzuia maendeleo ya vizazi na vizazi.

Kwa Hiyo mawazo mazuri kama haya uliyoyatoa Kwa Tanesco viongozi wengi hawana na hawataki hata kujishughulisha zaidi ya kuwaza mambo Yao binafsi.

Kwa namna hii nchi yetu itachelewa sana kusonga mbele kwani wanaopewa nafasi wanapewa kama fadhila ili nao wanufaike kupitia urefu wa kamba zao lakini sio Kwa ajili ya kujenga Nchi kiuchumi.
 
asee ni hatari sana
 
Mi napingana na mawazo yako.
Kufanya hivyo ni kuendekeza umasikini na kuulea na kuukomaza
 
Waue biashara ya mkaa na gesi kwa kumshusha garama za umeme hadi robo ya Sasa ilibwatumiaji wengi waongezeke na iokoe misitu na ku boost uchumi haraka kwa multiplayer effect itokanayo na Wingi wa umeme tukio nao sasa
 
Mawazo ya ki-socialism haya, hapa lazima taxation iongezeke, kila mtu abebe mzigo wake binafsi sikubalaini na hili wazo, hii italazimika watu wakatwe tozo kama vile kwenye REA
mbona hakuna sehemu aliyosema kodi iongeze mkuu? kwani unafikiri serikali haiwezi kuweka Ruzuku huko? kwani TANESCO wakifungia watu umeme alafu wakawakata kwenye LUKU hizo tozo zitatoka ziende wapi? kwani kimsingi si ilitakiwa jukumu la tanesco liwasambazie watu umeme bure ili watu walipie huduma? mfano sasa hivi ukitaka kufunga umeme unaambiwa ununue nguzo hata kama site yako haihitaji nguzo. Nafikiri mdau ameangalia pande zote na sioni sababu ya wewe kulipia tozo ili ulipe deni la mtu
 
Waue biashara ya mkaa na gesi kwa kumshusha garama za umeme hadi robo ya Sasa ilibwatumiaji wengi waongezeke na iokoe misitu na ku boost uchumi haraka kwa multiplayer effect itokanayo na Wingi wa umeme tukio nao sasa
Kweli kabisa mkuu mawazo mazuri
 
Mawazo ya ki-socialism haya, hapa lazima taxation iongezeke, kila mtu abebe mzigo wake binafsi sikubalaini na hili wazo, hii italazimika watu wakatwe tozo kama vile kwenye REA
Onyesha namna kodi itakavyoongezea kwa ku refer andiko langu Mkuu.
 
Sijui unaongea kitu gani, kutekeleza hili tanesco itahitaji fund, tanesco na mashirika mengine ya serikali uhai wao ni ruzuku ya serikali, serikali sio mzarishaji asilimia kubwa ya pesa ni Kodi na mikopo ya nje Kwa kiasi kikubwa.

Kuanzisha mradi mkubwa kama huu, Tanesco monopoly company, inayotangaza hasara kila mwaka halina uwezo WA kufund huo mradi ndio maana hata miradi ya uzalishaji WA umeme huwa ni pesa ya serikali na sio kampuni.

Kwa maana hiyo pindi mpango WA kuunganisha umeme bure ukianza bajeti ya serikali lazima iongezeke na hapo ndipo baadhi ya vitu kuongezwa Kodi na uanzishaji WA tozo mbalimbali unapoibuka na kiwango cha uombaji WA mikopo kitaongezeka,

We unadhani bila msaada WA marekani na Makato ya REA watu wanaponunua umeme tanesco wangeweza kusambaza umeme vijijini Kwa faida/hasara wanayozalisha?

Kwa hiyo ni wateja wa-Tanesco nchi nzima wamepewa mzigo WA kuchangia REA ili umeme uende vijijini.

Kumbuka kipindi tozo za miamala zilipoanza ni kipindi serikali ya mama ilipopandisha madaraja watumishi WA serikali ghafla baada ya kifo cha magu wakati sekta nyingi zilikuwa hazijatengemaa na hapo uchumi ulikuwa unakuwa Kwa 2%

Na huu mradi ukianza Hilo shirika halitoweza kusimama lenyewe bila msaada WA ziada WA serikali, vijijini unakuta nguzo imepita nje ya nyumba na MTU haungi umeme.

Pia vijijini MTU alieunganisha umeme anaweza akabaki na umeme WA 10,000 hata miezi miwili. Huu ni umeme WA REA. Imagine itachukua miaka mingapi Hadi kumaliza deni la kuunganisha umeme liishe.

Na hapo ndipo hasara inaendelea kukua wakati huo serikali inalazimika kuipa pesa shirika ili liendelee kufanya kazi

Tanzania sio tena socialist economy, na wala sio tena Tanzania tunayohitaji, mfumo wowote WA uchumi unaoweza mfanya MTU Fulani atozwe kitu zaidi Kwa ajili ya kutoa kitu Fulani mtu mwingine bure sio sawa
kwani akija kununua tena si anakatwa mkuu? au huo umeme wa elfu kumi atautumia kwa mwaka mzima? na hapa serikali inaweza tu kuangalia wale wenye uhitaji alafu wameshindwa kulipia gharama za kuunganishwa
 
Tanesco wako comfortable, hawana mshindani, la sivyo wangetia mkazo kuongeza wateja wapya zaidi.

Kila goli mama lingesaidia kuunga umeme kwa watu wengi waliokwama kwasababu ya kipato.
 
Ndio maana nimekuuliza itachukua miaka mingapi deni kuisha?

Kwa maelezo mtoa mada bei ya kuunganisha ni 337k/60m, na anasema vijijini walipe 5000 Kwa mwezi Kwa miaka mitatu, yaani hiki kiwango kilichotajwa Tu kina shida.

Maana Kwa mwaka mdaiwa WA kijijini atalipa 60,000, ndani ya miaka mitatu kiasi kitakacholipwa ni 180,000 hapo itadaiwa 157,000 we huoni kuwa ni hasara hii.

Yaani serikali na tanesco wakifuata huu ushauri shirika litakufa kama serikali haitolazimisha kuongezwa Kodi na tozo ama kuchukua mikopo toka wahisani

Hao wenye uhitaji unawapimaje?

Kulipa deni mteja analazimika WA kijijini atalazimikq kulipa 9400 Kwa mwezi bila Riba.

Haya umeme WA REA akinunua WA 5000, ili alipe deni kila mwezi na anunue umeme itabidi awe analipa 14,400.

Mzee, kama umewahi kuishi vijijini hiki kiwango ni cha hanasa. Watakaokuwa na uhitaji Kwa kuwa na uwezo WA kulipa ni wananchi baadhi ya wanaoishi senta ya kijiji hasa wenye maduka, lakini wale nje ya senta kamwe hatothubutu. Na wala haimainishi kuwa ahitaji umeme.
Kwani kazi ya TANESCO ni nini? yaani wao kama watoa huduma si ndio wanatakiwa waniletee huduma mimi nilipie huduma? kwanini mteja alipie miundombinu? mbona wakati wa JPM waliweka 27,000 na ikawezekana? tanesco wana jukumu la kuwaplekea wananchi huduma bure wao walipie wanachotumia tu.
 
Umeelewa maelezo yangu kiongozi na mzizi WA Mada uliyonijibu hapo nyuma na sababu ninazozitoa? La kama ungenielewa concern yangu na maelezo yooote wala hata usingeuliza kuhusu magufuli, na bado maswali ninayokuuliza hujibu
ok sawa mkuu
 
Back
Top Bottom