Serikali iwe makini, Urusi imekuja na mbinu hizi kuchukua vijana wa Kitanzania kwenda kupigana Ukraine

Serikali iwe makini, Urusi imekuja na mbinu hizi kuchukua vijana wa Kitanzania kwenda kupigana Ukraine

Mkuu, Hawajazuiwa. Ni vigezo na masharti tu kuzingatiwa. Ila hata unapoajiriwa hapa Tz huwa unapewa JD. Kinachofanyika katika uzi huu ni kuwapa Tahadhari wale wanaowania au kuwa-instigate (kuChochea na kuhamasisha) wenzao waende wakajiunge huko. Serikali kama Mamalka, inao wajibu wa kuhakikisha Usalama wa Raia wake. Mtoa mada tunamshukuru anaikumbusha Serikali itimize wajibu wake huo wa Kikatiba. Lakini kwa vijana wanaotaka kwenda mbona ni rahisi tu? WAENDEEEE. Nakumbuka kuliwahi kutolewa Tangazo la Wito kujiunga na Jeshi la Urussi.

Nadhani hilo tangazo halijafika kwa wengi. Wapo waliokata tamaa wapo radhi wakafie vitani KWA faida ya familia zao kuliko kufa njaa nyumbani.
Pana mtoto wa ndugu yangu alimaliza IFm ni Mhasibu jeshi la Uingereza yupo kwenye submarine ana ACCA chartered accountant.
 
Safi.Bila shaka alikaa akatafakari kwa kina kisha akafanya maamuzi huku akizingatia pia usalama wake. Hakukurupuka tu kwa sababu eti kuna hela nyingi. Hata askarri vitani huwa wanajali pia kwanza usalama wao na sio kufyatua risasi tu eti adui yuko mbele.
 
kule nasikia vyuo karibu na bure, ila ujue utakuja akili yako ina matege - warusi si wa kuchezea.
Uko sahihi 100%. Wataalam wa ki-Tz waliosomea fani zao Urussi ni Watata sana na hawaambiliki. Nimewahi kufanya nao kazi Serikalini; vichwa vyao wanajijua wenyewe. Matusi ni ya hapa na pale, wengi ni walevi kupindukia(Sio wanywaji) halafu madharau ni kwa sana. Kila kitu wanajua wao. Sijui huko wanalishwa nini wanapokuwa vyuoni Urussi.
 
La hasha . Ni hiari yenye hadaa. Anawalaghai i.e. anawawekea chambo(Bait). Tahadhari kabla ya hatari. Waende tena kwa wingi wao lakini wakiwa wanajua kwamba na hilo linaweza likawepo. Wasije baadaye kulia-lia hapa.
Hakuna chambo hapo. Hakuna ataepelekwa vitani kwa nguvu wakifika huko. Ataekwenda vitani ni yule atakae kwa hiyari yake tu.
 
Siku za karibuni nimekuwa nikiona matangazo mengine matandaoni ya kuwavutia vijana kwenda kusoma bure Urusi.

Kabla ya vita hii inayoendelea sikuwahi kuona matangazo kama haya

Sasa ukitazama kuna vijana kadhaa kutoka Afrika waliokuwa wanasoma huko wamefia vitani halafu wote walikuwa jela

Hii inaleta wasiwasi mkubwa, bahati nzuri watu wengi wamestuka ila wapo wajinga wachache wanaoweza kuingia mtegoni, serikali iwe makini

View attachment 2500583View attachment 2500584View attachment 2500585View attachment 2500587View attachment 2500592
Wewe wakichukuliwa unaumia nini!?
Kwanza serikali inasisitiza vijana wajiajiri na watumie fursa hizo ndio fursa zenyewe acha vijana wapambanie
 
Uko sahihi 100%. Wataalam wa ki-Tz waliosomea fani zao Urussi ni Watata sana na hawaambiliki. Nimewahi kufanya nao kazi Serikalini; vichwa vyao wanajijua wenyewe. Matusi ni ya hapa na pale, wengi ni walevi kupindukia(Sio wanywaji) halafu madharau ni kwa sana. Kila kitu wanajua wao. Sijui huko wanalishwa nini wanapokuwa vyuoni Urussi.
Vodka.Halafu wengi hawana maendeleo zaidi ujuaji na kuzeeka na utaalamu wao tu
 
[emoji444]Buffalo soldiers, stolen from Africa goes to America fighting for survival [emoji445]

[emoji444]Woi yo yo yo, Woi yo yo yo yooooooo[emoji444]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Safi.Bila shaka alikaa akatafakari kwa kina kisha akafanya maamuzi huku akizingatia pia usalama wake. Hakukurupuka tu kwa sababu eti kuna hela nyingi. Hata askarri vitani huwa wanajali pia kwanza usalama wao na sio kufyatua risasi tu eti adui yuko mbele.
Hilo Tangazo, kama Mods wataridhia, wanaweza kulipandisha tena hapa.
 
Serikali imepiga marufuku watanzania kujiunga na jeshi la mchi nyingine
Yeah. Serikali ipo makini sana kwani hiyo vita ikiisha na wao kurudi (kwa watakaosalimika)hapa nyumbani watafanya shughuli gani?? Si watajiingiza kwenye makundi ya kigaidi kama walivyozoea huko Urussi?
 
Mkuu siwezi umri umeenda am above 35yrs of age, ila ningekua below ningeenda hiyo in bonge la dili, sio kila mwanajeshi anaenda front line, hapana kuna department nyingi na enda kwenye section nzuri kupunguza chances of death ya vitani.
Usiwe mjinga pale Wagner hujipangii unaenda kitengo gani. Na hawana heavy weapons kazi zao nyingi ni infantry. Pia kwa 35yrs hujachelewa hata kidogo, Wagner wa miaka 40 na zaidi wapo. Nenda ufe maana hilo kundi halina haki wala sheria wala fidia, kama fidia ipo uliza ya Tarimo iko wapi na ya Nyirenda yule Mmalawi iko wapi.

Wagner hata kikosi kizima kifyekwe hakuna shida kwani hata katiba ya Urusi haitambui mercenaries. Kazi ngumu kama kupigana Bahkmut wanapewa wao. Ndio wenye casualties nyingi kuliko jeshi la nchi
 
Nafikiri kwenda kupigana urusi ni afadhali kuliko kufia hapa Tanzania kwa hizi tozo
 
Hapo ubaya uko wapi? Wewe hujui maisha naona, watu wengi hapa Africa wanatamani kujiuga na jeshi la Urusi ukipewa hiyo Fursa, mbona ni bonge la dili, kifia uko ni bahati mbaya tu.
Nenda uone kama utarudi
 
Wewe wakichukuliwa unaumia nini!?
Kwanza serikali inasisitiza vijana wajiajiri na watumie fursa hizo ndio fursa zenyewe acha vijana wapambanie
Kwa mtindo huo, vijana watakuwa wameajiriwa sio wamejiajiri. Ukiajiriwa unafuata na kutii maelekezo na amri ya aliyekuajiri. Tofauti na hapo, kama mwajiri wako ni Wagner group unanyofolewa naniliu yako chap na kutelekezwa hapo ujifie kwa kihoro. Kipaumbele cha Wagner kwa sasa ni frontline ya Bakhmut.
Ukijiajiri unao uhuru wa kupanga na kufanya au kutofanya i.e. Unafanya vile unavyotaka iwe kwa hiari yako au kwa msukumo wa matakwa ya ajira yako na mahali ulipojichagulia ajira yako iwe.
 
Acha wapambanie fursa
 
Back
Top Bottom