Serikali iweke taa za barabarani katika majiji yote makubwa nchini

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Katika miji yote mikubwa utakuta taa za barabarani zipo barabara chache na nyingi Ni mbovu haziwaki na hakuna ukarabati wowote.

Hakuna ufuatiliaji wala uongezwaji wa taa katika barabara kuu na halmashauri hazijishughulishi na hilo wanachojua wao mwisho wa mwezi uhakika basi imetoka hiyo.

Jiji kama la Dar es Salaam pekee ndo angalau miundombinu ipo vizuri pamoja na taa za barabarani ukilinganisha na mikoa au majiji mengine

Hata katika stand nyingi za Mikoani ni taa mbili tatu utakuta ndo zinawaka hivyo kusababisha kuwa kichaka cha vibaka na wezi wakati wa usiku.

Ni vyema Serikali kwa mambo madogo madogo na ya Muhimu kama hayo wakayapa kipaumbele badala ya mji kuwa na muonekano wa giza kila mwaka.
 
Nimefika kule Musoma nikashangaa kuna taa za barabarani na zinawaka kwa mafungu ila (out of topic) nimeshangaa mpaka sasa bado kuna mgogoro wa malipo ya wakaazi wanaotakiwa kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa pale.
 
Jineva off Afrika kama Igusule...mzee wa kibandiko sikia hii...lango la Ngaramtoni kama Isunga Ngwada
 
Halmashauri na manispaa zinahusika hapa kwa maana ya madiwani na mameya wao
 
Katika miji yote mikubwa utakuta taa za barabarani zipo barabara chache na nyingi Ni mbovu haziwaki na hakuna ukarabati wowote.

Hakuna ufuatiliaji wala uongezwaji wa taa katika barabara kuu na halmashauri hazijishughulishi na hilo wanachojua wao mwisho wa mwezi uhakika basi imetoka hiyo.

Jiji kama la Dar es Salaam pekee ndo angalau miundombinu ipo vizuri pamoja na taa za barabarani ukilinganisha na mikoa au majiji mengine

Hata katika stand nyingi za Mikoani ni taa mbili tatu utakuta ndo zinawaka hivyo kusababisha kuwa kichaka cha vibaka na wezi wakati wa usiku.

Ni vyema Serikali kwa mambo madogo madogo na ya Muhimu kama hayo wakayapa kipaumbele badala ya mji kuwa na muonekano wa giza kila mwaka.
Serikali hii hii ya CCM?
 
Wanakusanya kodi chungu nzima Kwanini wasiweke taa za barabarani hadi mtaani?

Watu usiku wanaendesha kwa kututusa tu kiasi afya ya macho kuweza kuwa shakani [emoji851][emoji848]
 
Taa za barabarani zipo shinyanga.. Pale wamejitahidi sana
mwaka 2020 zilikuwa zinawaka zote hadi raha kupita pale,mwaka 2021 mwishoni nimepita hapo inawaka moja hapa nyingine paleeeee nyingine kuleeee...nilipita mida ya saa 2 kasorobo usiku labda zilikuwa hazijawashwa/waka zote
 
Back
Top Bottom