Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,660
- 3,501
Kama ilivyo kawaida yangu,
Niliuliza kwanini kwenye uandikishaji wa wapiga kura watu wanarahisishiwa kwa kufuatwa kwenye vitongoji vyao na mambo yanaenda vizuri tu lakini kwenye swala la namba ya NIDA hawataki kuwasogezea wananchi huduma kwenye vitongoji vyao
Nikajibiwa NIDA ni swala nyeti hivyo nisifananishe na mambo ya upigaji kura (mjibuji alitamka "usifananishe mambo ya siasa na maswala nyeti ya kitaifa"). Jibu hili sikuridhika nalo na hatahivyo sijalipata kutoka kwa wenye mamlaka. Sasa nina ushauri huu
1. Kama ni maswala ya kiusalama kama alivyonijibu yule jamaa basi nashauri mtu kupata namba utaratibu ubaki huohuo uliopo lakini kuwekwe kipengele cha kuhariri taarifa ambapo mtu ataweza kuhariri taarifa zake yeye mwenyewe kwenye mfumo bila kulazimika kwenda wilayani milolongo kibao
2. Kama ni vinginevyo basi rahisisheni huduma itolewe kwenye vitongoji kila baada ya muda fulani watu waweze kusajiliwa, kurekebisha taarifa zao za NIDA nk kama inavyokuwa kwenye daftari la kudumu. Tofauti itakuwa ni hii... kwenye daftari la kudumu la wapigakura zoezi linafanyika kwa muda maalumu tu lakini kwenye nida ofisi wilayani zinakuwa wazi muda wote ila ni kwa muda maalumu tu kipindi fulani huduma inapatikana vitongojini
Ushauri huu nautoa kwa sababu naona tabu watu wanazopata kwenye documents zao pindi linapokuja swala la namba ya NIDA.