Serikali iweke wazi kuwa kwa sasa hakuna utekelezaji wa sera ya elimu bure

Serikali iweke wazi kuwa kwa sasa hakuna utekelezaji wa sera ya elimu bure

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
16,871
Reaction score
39,881
Hii sera ya elimu bure ilikufa na Magufuli. Kwa sasa elimu katika shule za umma ni gharama kubwa kuliko hata binafsi.
  • Bila Tsh 600,000 mtoto haanzi kidato cha kwanza.
  • Wazazi wananunua madawati, viti, meza, chakula, nk.
  • Wazazi wanalipa pesa za walimu wa kujitolea maana walimu hawatoshi.
  • Wazazi wanalipa pesa ya maabara kwa ajili ya mafunzo na vifaa.
  • Wazazi wanalipa pesa za walinzi.
  • Wazazi wanalipa pesa ya tuition.
  • Wazazi wanalipa pesa za vitabu vya shule, chaki, nk.
  • Wazazi wanaombwa pesa mno na walimu.
Serikali haitoi ruzuku kuendesha shule, shule hazina hata pesa ya luku, chaki, mipira, nk.

Serikali semeni wazi kuwa elimu ni ya kulipia na tangaza ada ambayo ni sawa (uniform) kwa wote, ili wazazi tulipie.

Mbona huko kwenye afya tunajua sio bure, na huwa tunagharimia gharama za matibabu bila kelele?!
 
Kwenye shule za msingi nako ni kero.
Jirani amepeleka watoto wa wawili kuanza darasa la kwanza, hapo shule ya msingi Makilagi, Mza na watoto wamerejeshwa. Vinatakiwa.

1.hela ya uji 6000 kwa mwezi, sharti ilipwe miezi 2.
2. Track suit tsh 23000
3. Fagio la kununua. Mtoto wa miaka sita na fagio refu la nje.
Watoto wamerudi nyumbani, wamekosa mahitaji. Mzazi naye kama watanzania wengine...
 
acha propaganda amna shule wanalipa laki sita
Hujui kuwa shule wanafunzi wanaenda na meza na kiti 150k
Pesa ya mlinzi 100k
Pesa ya chakula na uji 150
Pesa ya laboratory 100k
Tuition 100k
Pesa ya chako 40k
 
Hujui kuwa shule wanafunzi wanaenda na meza na kiti 150k
Pesa ya mlinzi 100k
Pesa ya chakula na uji 150
Pesa ya laboratory 100k
Tuition 100k
Pesa ya chako 40k
acha propaganda hakuna anelipa hizo cost zote, wewe kama umekosa hoja kalale
 
Back
Top Bottom