HOJA Serikali iweke wazi namna watakaohitimu NTA Level 7 watakavyotambuliwa katika mfumo wa ajira, madaraja na mishahara

HOJA Serikali iweke wazi namna watakaohitimu NTA Level 7 watakavyotambuliwa katika mfumo wa ajira, madaraja na mishahara

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
sau.jpg
Nimeona Wizara ya Afya imeanzisha programu za Higher Diploma (NTA Level 7) katika maeneo ya Anaesthesia kupitia MWACHAS, na Midwifery kupitia MUHAS. Hili ni jambo zuri na hatua kubwa katika kuimarisha wataalamu wa afya nchini.

Hata hivyo, kuna jambo muhimu linalohitaji ufafanuzi wa haraka kwa watumishi na wanaotarajia kujiunga na programu hizi. Mpaka sasa haijawekwa wazi muundo wa utumishi na namna watumishi watakaohitimu NTA Level 7 watakavyotambuliwa katika mfumo wa ajira, madaraja na mishahara. Watu wanaenda kusoma bila kujua baada ya kumaliza watawekwa katika kada gani, watapandishwa daraja au la, na sifa zao zitatambulika vipi katika mfumo wa Serikali.

Kwa upande wa Anaesthesia, changamoto ni kubwa zaidi. Kuna watumishi ambao wamepata training ya mwaka mmoja ya Anaesthesia, lakini bado kuna changamoto ya utambuzi rasmi wa qualification hiyo kwa sababu hakuna chombo/baraza maalum... linalosimamia na kutambua taaluma hiyo kwa namna ilivyo kwa kada nyingine.

Hii inawaweka wataalamu hawa katika hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu maendeleo yao ya kitaaluma, ajira, madaraja na maslahi yao baada ya mafunzo.

Kwa hiyo, tunaomba Wizara ya Afya, TAMISEMI, PO-RALG na mamlaka husika kutoa muundo na mwongozo rasmi mapema kuhusu: utambuzi wa Higher Diploma NTA Level 7, kada na salary scale watakazowekwa wahitimu, uwezekano wa promotion kwa watumishi waliopo, pamoja na utambuzi na usimamizi wa wataalamu wa Anaesthesia waliopitia mafunzo ya mwaka
 
Back
Top Bottom