Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mpaka hivi sasa tunavyoongea, Mwenyekiti Mbowe hajawahi kusafishwa na mahakama wala serikali wala chombo chochote nchini kuwa tuhuma za serikali kwa Mbowe kuhusu Ugaidi zilikuwa za uwongo. Sisi wananchi tunachoamini ni kuwa kesi hiyo ilikuwa ni ya mchongo, ya kubambikiza na ya uonevu. Lakini kama huo ndiyo ukweli wa hiyo kesi, kwa nini Mwenyekiti Mbowe hajawahi kufungua kesi ya madai ya kudai fidia au kutaka jina lake lisafishwe kwa kubambikiziwa kesi feki?.
Mbowe hakuachiwa na mahakama kwa sababu alishinda kesi, bali aliachiwa na mahakama kwa sababu serikali iliamua kutoendelea na kesi. Serikali ikiamua kutoendelea na kesi haimaanishi kuwa ilichokuwa ikishtaki nacho ni cha uwongo pekee, bali inaweza kuwa ni kwa sababu nyingine ambazo yenyewe inaona zinafaa.
Mimi naamini ile kesi ni ya mchongo, lakini huwa sipendi kumpa mtu benefit of doubt kwa asilimia 100. Ningependa kujua kwa nini SERIKALI HAIJAMSAFISHA MBOWE katika TUHUMA ILIZOMPA?. Maana maana mtu akiachiwa kwa NOLE PROSEQUI haimaanishi hana hatia, bali kesi inaweza kufunguliwa upya na ikaendelea.
Je kutokana na kuachiwa kupitia Nole prosequi Mwenyekiti amekuwa compromised?, Kwamba serikali ina ushahidi mkubwa dhidi yake na hivyo inamblackmail kuua upinzani wa kweli nchini?.
Au Je serikali ina mafaili mengi ya mwenyekiti kwa hiyo salama yake ni kuwa msaliti wa mabadiliko ya kweli nchini?