concordile 101
JF-Expert Member
- Oct 13, 2013
- 3,379
- 6,624
nakubaliana nawewe ila kabla hatujaenda mbali, ili tufanikiwe kwenye kilimo sharti serikali au sheria ambazo zinazuia watu wasivutikike kuwekeza kwenye kilimo zifutwe.Sijakubaliana na wewe unaposema maji tatizo nchini ila nimekipenda hicho kipande nilicho-qoute.
Ingawa ni ukweli kwamba wakulima wengi wanategemea convenient sources of water ambazo zitawapa urahisi wa kufanya shughuli za kilimo bila gharama za ziada. Na vyanzo hivi ni mito ambayo kama ulivyosema inategemea mvua hivyo kama hakuna mvua hakuna mito.
Potential and reliable sources of water nchini ni nyingi sana. Nafikiri Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zinazoongoza kuwa na vyanzo vingi vya maji baridi. Tuna maziwa makuu matatu: Tanganyika, Nyasa na Victoria (kama wale jamaa wa jangwani wasipoleta figusu).
Ukiachana na nayo ingawa sina taarifa sahihi lakini nafikiri tuna moja kati ya aquifer kubwa sana zilizohifadhi maji ardhini. Nasema hivyo sababu almost everywhere Tanzania unaweza chimba na kukuta maji ingawa sehemu nyingine yanaweza yasifae kwa umwagiliaji kutokana na excess amount of salt contents.
Mfano hai. Katika jimbo la Nebraska, USA kila siku galoni bilioni 7.3 ambayo ni 94% ya maji yanayotoka ardhini yanatumika kumwagilia ekari milioni 8.5
Kwa kuhitimisha ni kwamba tuna vyanzo mbadala vingi vya maji isipokuwa kunahitajika uwekezaji mkubwa. Ni kama vile serikali au sekta binafsi itumie mabilioni kuvuta maji toka maziwa makuu hadi sehemu husika. Ndio, inawezekana kama ambavyo imewezekana kuvuta maji toka ziwa Victoria hadi shinyanga, tabora na maeneo ya jirani. Nina hakika hilo likifanyika its impact on agricultural sector will be astonishing.
mfano mdogo ni zuio la kusafirisha chakula nje. kwa ujumla hatuhitaji kwanza kupata wawekezaji toka nje kuja wekeza kwenye viwanda vya usindikaji kwanza , inatupasa serikali iweke mazingingiara ya raia wake kuweza kupata mitaji kwa kuuza mazao watakavyo ili huko baadae wapate mitaji ya kufungua miviwanda mikubwa.
sasa hivi kuna excess ya mahindi mengi sana nchini, imefikia hatua mpaka hatua kwa kilo unatafuta mteja umuuzie kwa kwa 300 tsh lakini hata hiyo haumuoni, lakin upande wa pili tu hapo kenya somalia ,congo rwanda na kwinigne kuna uhitaji mkubwawa hii bidhaa na kwa bei nzuri lakini serikali imebana.
kinachohitajika sio lazima serikali ijenge miundo mbinu ila iweke mazingira tu ya mkulima kunufaika watu wazawa watawekeza tena zaid hata ya hiyo.
mfano mdogo kwenye picha hapo juu ya lateral irrigational systems, niliwahi jaribu kuwacheck jamaa flan wa turkey kujengewa hiyo bei ilikuwa almost 8000- 13000 usd kwa 100meter. urefu wake zinaweza kwenda mpaka mita 1300 ambayo ni almost bei ya yutong moja ukiweka na usafiri au letsay ufanyiwe turnkey project ni almost yutong tatu, lakini waweza mwagilia mpaka hectare 1000. kuhusu maji kiukweli underground water sisi nadhani tunayo ya kutosha na sio haihitaji mpaka mtu awe na mabilion , kuna mzee mmoja singida anatumia maji visima na ana almost acre 60 za vitunguuu. kwa makadirio tu sidhani kama mtu size ya sumry au dar express anashindwa kuchimba ya kumwagilia acre 5000. kinachosumbua tu.
-serikali zetu wamejazana watu ambao hawana vision
-serikali zetu kuna watu wanafanya biashara ila hawachez fair game, so ni vigumu sana kukubaliana na vitu ambavyo vitaleta mgongano wa kimaslahi( mfanno refer.to sumry kucompete na mtu anae jaza mafuta tu halipi kodi wala fine zaid rejea kwenye zuio la mtu flani kuzuiwa kujenga hospitali ya moyo arusha)
- siasa