Serikali iwekeze katika sekta ya kilimo na hasa Kilimo cha umwagiliaji

nakubaliana nawewe ila kabla hatujaenda mbali, ili tufanikiwe kwenye kilimo sharti serikali au sheria ambazo zinazuia watu wasivutikike kuwekeza kwenye kilimo zifutwe.
mfano mdogo ni zuio la kusafirisha chakula nje. kwa ujumla hatuhitaji kwanza kupata wawekezaji toka nje kuja wekeza kwenye viwanda vya usindikaji kwanza , inatupasa serikali iweke mazingingiara ya raia wake kuweza kupata mitaji kwa kuuza mazao watakavyo ili huko baadae wapate mitaji ya kufungua miviwanda mikubwa.
sasa hivi kuna excess ya mahindi mengi sana nchini, imefikia hatua mpaka hatua kwa kilo unatafuta mteja umuuzie kwa kwa 300 tsh lakini hata hiyo haumuoni, lakin upande wa pili tu hapo kenya somalia ,congo rwanda na kwinigne kuna uhitaji mkubwawa hii bidhaa na kwa bei nzuri lakini serikali imebana.
kinachohitajika sio lazima serikali ijenge miundo mbinu ila iweke mazingira tu ya mkulima kunufaika watu wazawa watawekeza tena zaid hata ya hiyo.
mfano mdogo kwenye picha hapo juu ya lateral irrigational systems, niliwahi jaribu kuwacheck jamaa flan wa turkey kujengewa hiyo bei ilikuwa almost 8000- 13000 usd kwa 100meter. urefu wake zinaweza kwenda mpaka mita 1300 ambayo ni almost bei ya yutong moja ukiweka na usafiri au letsay ufanyiwe turnkey project ni almost yutong tatu, lakini waweza mwagilia mpaka hectare 1000. kuhusu maji kiukweli underground water sisi nadhani tunayo ya kutosha na sio haihitaji mpaka mtu awe na mabilion , kuna mzee mmoja singida anatumia maji visima na ana almost acre 60 za vitunguuu. kwa makadirio tu sidhani kama mtu size ya sumry au dar express anashindwa kuchimba ya kumwagilia acre 5000. kinachosumbua tu.
-serikali zetu wamejazana watu ambao hawana vision
-serikali zetu kuna watu wanafanya biashara ila hawachez fair game, so ni vigumu sana kukubaliana na vitu ambavyo vitaleta mgongano wa kimaslahi( mfanno refer.to sumry kucompete na mtu anae jaza mafuta tu halipi kodi wala fine zaid rejea kwenye zuio la mtu flani kuzuiwa kujenga hospitali ya moyo arusha)
- siasa
 
Umeandika mengi sana ya msingi. Na ninakubaliana na wewe katika hayo yote. Na hapo juu sikuhusisha serikali pekee juu ya ujenzi wa miundombinu, sekta binafsi ina nafasi kubwa ya kufanya nchi hii kuwa net exporter wa bidhaa za kilimo. Tuna kila sababu ya kufanikisha hilo. Lakini bado mwamko ni mdogo kwa hao watu binafsi ingawa sera za serikali za kuzuia kutoa mahindi nje zinakatisha sana tamaa(hili hata mimi limenikumba)
Lakini nafikiri tuna tatizo Ia kung'ang'ania aina moja ya zao. Tunaweza lima in large scale ngano, pamba, maharage, mchele, tunaweza lima kwa wingi na kutengeneza animal feed ili tupate faida indirectly kwa ku-export nyama ya ng'ombe, nguruwe na hata jamii ya kuku.
Kifupi fursa za kilimo bado zipo nyingi ila pale juu serikalini tunahitaji watu wenye vision and passion ya kuona vyanzo vingine vya kutukwamua kiuchumi. Hili bado sijaliona africa na hata kwa vyama vyetu vya upinzani.
 
Serikali imewekeza billion 41 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Chato alafu wanaCCM wanakenua tu kama ngiri
 
Umeona ambali laiti wasira angeona kama wewe sasa hivi tungekuwa tunaongelea economic boom
GDP ingekuwa ya kiwango cha lami

Tena nchi yetu imezungukwa na vyanzo vya maji pande zote NNE za dunia na mwambao wa bahari ya Hindi ndyo umevunja rekod kabisa kutoka Lindi mpaka tanga !yaani wazungu wanatucheka Tu

Pesa zinazotumika kufungua ma viwanda ya gharama zingewekezwa huku vijana wengi zaidi wangepata ajira sasa tutegemee population explosion mijini na uchafuzi wa mazingira na maongezeko ya majotro maana viwanda impact yake si ndogo

Kilimo kilimo kilimo kinaheshimika duniani kote na nchi zote tajiri duniani zililima kwanza kabla hata ya kuwa na viwanda
Dhana ya kilimo ni pana na kilimo huwa ukikianzisha kinazalisha na shughuli nyingne humohumo kama ufugaji tena wa kisasa maana kama unalima pamba utapata na chakula cha kulisha mifugo kama mashudu
 
Nakubaliana na wewe kabisa katika hoja yako mkuu, sheria zisizo rafiki kwa mzawa, masoko na sera mbovu na siasa chafu ni vikwazo vikubwa katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji
 
Safi sana mkuu hakika ushauri wako ni mzuri sana katika kuboresha sekta ya kilimo cha umwagiliaji
 
Mhh hapo kwenye large scale ndo penyewe ila kaka, kiukweli large scale haiwez kuja bila ya kuanzia chini. kuhusu muamko kaka upo sana kwa watu wengi sana ila sera mbovu. chukulia mfano mtu unalima pamba ila kuuza eti lazima uiuzie kampuni fulani. kwanini wanunuzi wasiruhusiwe kununua directly kununua pasipo ukiritimba kwa baadhi ya mazao. kuna baadhi ya mazao kama ngano tukiwa na sera madhubuti tunaweza uza mpaka tukachanganyikiwa kwa sabab hakuna nchi afrika ambayo inazalisha ngano kwa wingi. sio ngano kuna mawese au michikichi, almost nusu ya mafuta ya kula yanayozalishwa dunian yanatokana na michikichi, sisi huku tunanunua crude oil toka malaysia na indonesia kuja kusindika mafuta, na kwa dunian 78% ya mafuta yanatoka indonesia na malaysia tu.
napenda sana kilimo na nishajaribu zaid ya mara tatu ila nimeumizwa mara zote na sera mbovu. mahindi nilime mimi kuuza unipangie pa kuuza. daah
 
Tanzania maji si tatizo hata kidogo..... hatujawekeza vya kutosha katika sekta ya maji. Tanzania tuna maji mengi sana na hatuwezi kabisa kuyatumia.

Tuna water bodies za kutosha na tuna maji underground mengi sana na kila mahali tumeshindwa kuyatoa chini kuyaleta juu kwa matumizi.

Tanzania hatuna shida ya maji hata kidogo ni sisi wenyewe kuamua tu.
 
Ni wazo zuri.
Lakini unajua wazi kuwa hiki unachokisema hakiwezi kufanywa na hao ndugu zako. Asilimia ya bajeti inayopangwa hata theluthi haijawahi kufika kwa walengwa. Inaweza ikawwa billion 963 zikafika bilion 163 sasa hapo kuna kazi.
Sahau maendeleo kwa uongozi huu wa rushwa na mbwembwe.
 
Sawa, ila kwa pamba liko huru tu, unamuzia yeyote kokote. Kwa Simiyu labda kwa mikoa mingine.
 
Mkuu umenena jambo zuri. Malighafi kwanza,ndo viwanda vifuate. Sina uhakikaa kama utaeleweka na wengi. Kama ambavyo nimemsikia mtu mmoja akisema, unajenga uwanja wa ndege wa kisasa na ukishakamilika, unatafuta watumiaji wa huo uwanja ili uonekane hukutapanya fedha!
 
Mkuu tatizo kubwa ninaloliona Tanzania ya sasa,kuna watu wanalazimishiwa uongozi hata kama hawana uwezo. Wale wenye uwezo na creative wanawekwa pembeni hata kama huko nyuma walishaonyesha au kufanya mazuri tuu. Ilitakiwa Taifa lifungamane,tuwe na mambo endelevu siyo yale mazuri yaliyoletwa na usiyempenda yafunikwe . Issue ya kilimo cha umwagiliaji haijaanza leo,ni tangia ukoloni na Mwl. Nyerere aliendeleza sana. Mf. Shamba la mpunga la Mbarali na mengineyo. Leo hii,maeneo yale yanagawiwa wakulima wadogowadogo wasio na nyenzo yoyote kuyalima! Sasa hapo ni kwenda mbele au kurudi nyuma? Niliwahi kusikia mradi mkubwa wa umwagiliaji bonde la mto Rufiji,je umefikia wapi? Siku Mungu atatupa uwezo wa sisi Watz kukaa pamoja bila kupigana vijembe,kudharauliana,kutengana kwa vyama kuwa DED au DC atoke chama fulani hata kama hana uwezo ndipo maendeleo yatakwenda kwa kasi.
Juzi nimeona Marais 5 wastaafu wa kule Marekani wakikaa pamoja kuchangia mfuko wa maendeleo ya taifa lao. Niliona wivu sana na kujiuliza kulikoni Maraisi wetu wastaafu kutoiga hilo na kuendeleza mambo makubwa kama hili la Umwagiliaji? Mungu tusaidie tupate maono mazuri zaidi.
 
Mkuu kwanza hongera kwa Mada nzuri.
Nikijikita kwenye kuchangia, kama ulivyosema kuwa Kilimo kimeajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania lakini bado kuna changamoto lukuki ambazo ingekuwa ni vema zikafanyiwa kazi kwanza kabla ya kujikita kwenye mabadiliko ya Miundombinu ya Kilimo, baadhi ya Changamoto hizo ni:
i/ Zaidi ya asilimia 50 ya Wakulima bado wanatumia zana duni za Kilimo, bado hadi leo hii Wakulima wanalima kwa mazoea yani Kilimo cha kienyeji kuanzia kwenye Maandalizi ya Shamba, uchaguzi wa Mbegu etc, hivyo Serikali inabidi ianze kwa kuelimisha Wakulima juu Kilimo cha Kisasa ambacho ndo Kilimo chenye tija.
ii/ Kukosa Soko la uhakika la Mazao, pamoja na Wakulima kuzalisha kwa zana duni bado Soko ni tatizo, Mfano hadi sasa Wilaya ya Handeni Gunia la Kilo 100 halizidi Elf 45 na hapo ni zaidi ya miezi minne toka Mavuno, ikiwa miezi hiyo minne kabla ya Mavuno hiyo Elfu 45 ilikuwa ni bei ya Debe moja la Mahindi. Aidha si Mahindi tu hali ndo ipo hivyo kwenye Maharage Kunde, Ufuta na Mihogo.
iii/Urasimishaji katika Sekta ya Kilimo nalo ni tatizo lingine, Wakulima wengi wanakosa fursa za Mikopo kutokana na Sekta hiyo kutokurasimishwa.
iv/ Pamoja na scheme kutokuwepo nyingi lakini hata hizo chache zilizopo bado hazina manufaa kwa Wakulima, hazifuatiliwi wala hazijengewi uwezo ili ziwe na tija kwa Wakulima, casestudy ni Scheme za Same, Korogwe na Bagamoyo.
 
Pole sana mkuu. Tuna changamoto kubwa sana katika sekta hii. Nimevutiwa na hiyo taarifa ya mafuta.
 
Mtazamo na kipaumbele cha Rais kikiwa na kuhakikisha kilimo limefanikiwa na itakuwa hivyo. Shida ni Katiba ya nchi.
 
Mchango mzuri kwa wadau wa sekta ya kilimo.
 

View: https://www.instagram.com/p/DF72OBoo8pe/?img_index=1&igsh=MXJxZGU0bHkxczMwZg==
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…