Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Hamjambo wote!
Lazima Tafiti, chunguzi na tathmini zifanyike. Tujue Watanzania ni nini wamebarikiwa na kile wanachoweza kulifanya to the most. Kisha tungalie ni nini tunacho katika nchi yetu ambacho tunaweza kukitumia kuweza kuendelea na kuendeleza taifa letu kuwa taifa Kubwa zaidi.
Huwezi kuendelea kama hutumii kile ulichobarikiwa. Abadani! Hiyo haiwezekani.
Ulichonacho ni chako. Huwezi kukikopa kwa mtu mwingine.
Kitendo cha kutaka kutumia ambacho hauna ni Kutafuta kutawaliwa na wale ambao wanavyo hivyo unavyovihitaji.
Kutaka kutumia ambavyo huna na ukaacha ulichonacho ni kupoteza hata kile ambacho ulikuwa nacho.
kwenye uchumi na biashara, ili biashara iwe ya faida ni lazima utumie kwa ubora kile ulichonacho(mtaji) kupata kile ambacho hauna(faida) hiyo ndio biashara. Na lazima uendelee.
Kwenye biashara, lazima uone kile ulichonacho ni Bora Sana hata kama ni kidogo ili uweze kukitumia kwa ufanisi na Weledi. Ili ukipe thamani na kithaminiwe na watu wengine lazima ukithamini wewe Kwanza. Hayo ni Mambo ya uchumi na biashara.
Kitu(resource) hakiwezi kuwa na thamani(value) kama hakitapewa thamani na Watu. Kwenye watu kuna Makundi mawili. Kundi la Kwanza ni lile lililopewa resources hizo na kundi la Pili ni lile lisilokuwa na resources hizo.
Kuna resources ambazo zipo sehemu zote ikiwemo ardhi. Na kuna resources ambazo zipo sehemu chache.
Resources zilizo sehemu zote wenye Akili hutafuta namna ya kuzihodhi kwa sehemu kubwa na kuzimiliki ili kuzipa resources hizo thamani.
Kama serikali na hapa nazungumzia serikali ya Watu wote. Kwa sababu kuna aina mbili za Serikali. Aina ya Kwanza ni serikali ya Watu Wachache ambayo ni Kwa kimombo unaweza kuiita organised Mafia. Yaani Genge la wahuni ambao wako organised kuzuia wengine Fursa na wao kujineemesha wenyewe. Hizi ziko nyingi duniani.
Kwamba Yale mambo yote ambayo ni uhalifu serikali ya aina hii hufanya lakini wao huzuia wengi wasifanye. Mathalani, ufisadi, uuzaji wa madawa ya kulevya, uporaji, utekaji na mauaji n.k.
Ndio maana serikali hii inaitwa Organised Mafia..
Serikali ya watu wote hizi ni zile ambazo watu wote wapo chini ya Sheria. Mtu yeyote huweza kushtakiwa na kuhukumiwa bila kujali nafasi yake, kama KOSA limefanyika Basi Sheria hazitaangalia nafasi ya Mtu huyo.
Serikali hizi hufuata uchaguzi wa hiyari ya watu katika kuchagua viongozi wao.
Vyombo vya dola huwa kwaajili ya watu na sio kuwa na maslahi ya watu wa chache kama ilivyo kwa organised Mafia.
Ili rasilimali au Baraka zilizopo ndani ya nchi ikiwepo Baraka za Rasilimali watu pamoja na maumbile mengine ya Dunia ni lazima serikali iwe ya watu wote.
Hii italeta matumizi ya HAKI ya rasilimali pamoja na karama, uwezo, maarifa ya watu katika kuendeleza taifa husika.
Watanzania wamejaliwa mambo mengi lakini kubwa zaidi ni ardhi ya Kilimo na ufugaji kwa sehemu kubwa.
Ilikuwa muhimu baada ya kuweka miundo mizuri ya logistics na Usafirishaji, miundombinu ya Nishati ya Umeme, na huduma muhimu za maji ya uhakika kwa Watu wengi kama sio wote.
Na hapa sizungumzii Maji ya kunywa.
Nazungumzia Miundombinu ya Maji yanayotosha kwa mahitaji muhimu ya nyumbani na shughuli za uzalishaji kama Kilimo cha umwahiliaji, ufugaji wa samaki, na visima vya kuwanywesha mifugo ya wafugaji, majosho.
Kwa nchi Maskini inayokua, serikali haikupaswa kuwa hata na wazo la karibu kununua madege makubwa ya biashara.
Kwa sababu hasara ni uhakika na kufilisika ni Jambo lisilokwepeka.
Sababu zipo wazi na Wala hauhitaji kuwa na elimu Wala akili za kurusha rocket angani kujua kuwa Sisi sio Watu wa safari za ndege kutokana na uchumi wetu, culture zetu sio Watu wa kusafiri safiri,
Asilimia kubwa ya Watanzania sio Watu wa kupenda safari. Sio ajabu Nusu ya Watanzania wanaweza kukaa zaidi ya Miaka mitatu hawajasafiri kwenda hata Mkoa mwingine wenye umbali wa kilometres 300 tuu.
Ni Mpaka mtu aumwe, Afe, au aende kusoma.
Kwa vile Sisi tulichonacho mkononi kwa wakati huu ni ardhi kubwa ya Kilimo na watu wanaojishughulisha na Kilimo.
Serikali ingepaswa imulike huko zaidi
Mazao ya chakula na Yale ya biashara yangeongeza tija kwenye maisha ya Watanzania na pato La taifa lingekuwa.
Moja ya athari mbaya ya ukosefu wa ajira ni Watu kushindwa kutumia walivyo navyo na kuhangaika na vile ambavyo Hawana.
Kwenye Vita yoyote unatumia kile ulichonacho kwa wakati husika kama silaha kupambana na maadui zako.
Ni nini Tanzania tunacho, kitu gani Watanzania wanacho?
Watanzania tuna yafuatayo kwa wingi wetu
1. Ardhi ya Kilimo
2. Maziwa na Mito ya uvuvi
3. Maeneo ya ufugaji
Maeneo hayo matatu yanaweza kuajiri robo kama sio nusu ya Watanzania wote.
Kuanzia wakulima, wauza nafaka na chakula, madalali, walinzi, wauza mifugo, wavuvi, wauza mazao ya uvuvi, viwanda vidogo vya kuchakata malighafi za Kilimo,
Utengenezaji wa ngozi, vitu, mabegi, mikanda, n.k.
Maeneo ya Kati yatakayochukua Watanzania kwa kiwango cha Kati ni wenye Elimu za huduma kama Waalimu, Wanasheria, madaktari, wahasibu, mainjinia, n.k. hawa kimahesabu watakuwa chini ya robo ya watu wote.
Kundi Hilo serikali haipaswi kueneza Propaganda ya kuzifanya Kazi hizi ni Bora kuliko Kazi zingine. Ili kuondoa kasumba mbaya na kuathiri nguvu Kazi ya VIJANA.
Shughuli za Mikono na ufundi kama upishi, ushonaji, saluni, makeup, Michezo na burudani hutegemea zaidi kundi la Kwanza Kule la wazalishaji.
Kundi la uzalishaji linapokuwa chini ya kiwango tunatarajia makundi mengine yataathirika kwa Kiasi kikubwa Sana.
Kuanzia gharama za Maisha kuwa juu kutokana mahitaji ya msingi ya binadamu kama chakula kutokuwa na uhakika.
Serikali inaowajibu wa kutumia rasilimali za msingi tulizobarikiwa ili kujenga ngome na taifa lenye nguvu.
Baada ya hapo tukishakuwa na surplus ya kutosha Sera za UVAMIZI zianze kufanya Kazi.
Kuvamia mataifa mengine kwaajili ya kupeleka bidhaa zetu, mitaji yetu, watu wetu ili kuongeza faida zaidi na kuchukua faida na utajiri wa maeneo mengine ili kujiweka katika nafasi nzuri ya ku-sustain kwa Karne nyingi kama taifa
Mimi acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam