Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
Sasa hivi kuna changamoto kubwa ya uhaba wa mvua au mabadiliko ya tabia nchi. Serikali iwekeze kwenye kilimo cha umwagiliaji cha kisasa kinachotumia maji machache katika mashamba makubwa kwenye mikoa na wilaya ambazo zinafaa kwa umwagiliaji. Wananchi/vijana wapewe maeneo walime kwa kumwagilia. Na wawe wanatangaza kwa uwazi(bila connection au rushwa au kujuana na wakubwa) juu ya upatikanaji wa mashamba kwenye umwagiliaji. Labda pawe na system au website ya "umwagiliaji portal"
Pia wawekeze katika uzalishaji wa mbegu zinazostahimili ukame. Hasa mazao yenye uhitaji mkubwa kama Mahindi,maharage, ngano, mpunga , alizeti, njugumawe,choroko, dengu, mtama, uwele, ulezi, jamii ya mikunde n.k Hata pia zipatikane mbegu kwa ajili ya malisho ya mifugo. Maana wafugaji wa kuhamahama ndio wanaleta migogoro kwa kulisha mazao ya watu. Ndio maana kuna migogoro ya wakulima na wafugaji.
Hii Hali ya hewa kwa sasa haitabiriki. Ni bora kujipanga mapema na kujikinga na njaa. Na hizi siku za mwisho Yesu alisema patakuwa na njaa na vita. (Dalili za kurudi kwa Yesu mara ya pili.)
"Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. "
Mathayo 24 :7
Wengine ongezeeni maoni yenu