Poleni kwa mahangaiko ya dunia hii ndugu zangu. Poleni wahanga wenzangu mliopitiwa na wezi.
Ushauri kwa serikali: Kuna haja ya kuona namna ya kuweka mazingira wezeshi kwa wazee wa mila kuanzisha mahakama na kutoa hukumu kimila.
Katika kupambana na wizi au uhalifu katika jamii, baadhi ya nchi jirani wamewatumia wazee wa kimila. Wazee hao wanazo mahakama za jadi zinazoamua mashauri kwa haki.
Ni jambo la kawaida kabisa nchini Zambia, Malawi, DRC, n.k kukuta mtu anafanya biashara kubwa pembezoni kabisa mwa mji bila wasiwasi wowote juu ya wezi.
Ikitokea mtu huyo ameibiwa anaamua au apeleka shtaka lake polisi au kwa wazee. Mahakama za jadi huwezesha mtu kupata mali zake au wezi kupatiwa adhabu wanayostahili na kutoa funzo kwa wengine.
Ninewahi kuona kupitia TV station moja ya ndani wazee wakitumia mbinu zao za jadi kulinda vyanzo vya maji. Sikumbuki vyema ni wapi.
Kama kweli tunataka kusonga mbele na kufanikiwa katika ulinzi wa mali binafsi na za jamii, ni lazima kutumia njia zaidi ya moja. Kuendelea kutumia polisi na mahakama zilizopo (watenda kazi wengi kwenye vyombo hivyo ufanisi wao na weledi wao unatia shaka) ni kujikwamisha.
Ukipita mijini kuna matangazo ya matapeli yakisomeka "mganga wa jadi kutoka Sumbawanga, Kigoma, Nigeria anarudisha mali zikizopotea ...". Na watu wengi hutapeliwa katika kunusuru mali zao zilizoibwa. Si vyema kuwacheka au kuwadhihaki.
Miaka ya hivi karibuni, kwa kiasi kikubwa jeshi la polisi limefanikiwa kupambana na uhalifu wa kutumia silaha maeneo mengi ya nchi yetu.
Maeneo mengi kunashamiri wimbi la vibaka wanaovunja na kuiba mifugo, maduka, stoo za mazao n.k. Kila siku maisha yanazidi kuwa magumu na maadili kushuka, hivyo tutarajie ongezeko la wezi mara dufu. Uhalifu huu hudumaza jitihada za mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kujikwamua na umaskini.
Kwa mfano, mtu anakopa milioni 3 vikoba ili aboreshe mradi wake. Akileta tu mali, usiku vibaka wanapita na mzigo wote. Siku inayofuata anafikiria kupata hela ya kulipa rejesho, ili hali hana biashara.
Akitoa taarifa polisi, anaambiwa tutalishughulikia na atoe taarifa kama atapata habari juu ya waliomwibia. Ndio imetoka hivyo.
Ikitokea mwizi amekamatwa, atafungwa baada ya mlolongo mrefu wa kusikiliza shauri. Mwizi husika akirejea uraiani anaendeleza kazi yake ya wizi kwa umahiri zaidi. Wananchi wakimdaka wanamuua. Nguvu kazi inapotea, na ikiwezekana kuacha wategemezi wakiteseka, na pia mahakama kuelemewa na mzigo wa kesi.
Ikiwa kama tutaendelea kuwategemea polisi na mahakama pekee katika kukabiliana na vibaka hali itazidi kuwa mbaya, na itabidi kila mtaa kuwe na kituo cha polisi, na kila wilaya kuwe na gereza kubwa.
Tanzania haina dini, hivyo mapadri, wachungaji, masheikh n.k tuvumiliane katika hili. Polisi na mahakama msiogope kuhusu ajira na hadhi yenu.