Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Sisi Wakazi wa Kahama kiukweli tunayo kero ya barabara kutokuwa na ubora mzuri hali ambayo imekuwa ikitupa shida kwenye kutekeleza majukumu yetu.
Barabara za mjini takribani kote ni changamoto, mashimo mashimo kila kona jambo ambalo linahatarisha usalama wa vyombo vyetu kuharibika mara kwa mara, pia ni hatari kwa kuwa inaweza kusababisha ajali.
Kwenye mkoa mzima wa Shinyanga nadhani hapa Wilaya ya Kahama ni moja ya Wilaya inayochangia ukusanyaji wa mapato mengi mpaka kuna wakati ilisikika taarifa kuwa ilitakiwa kupewa hadhi ya Mkoa.
Natoa wito kwa Serikali kushughulikia hakikisha tunapata barabara nzuri kwa mashimo kuzibwa kwani wakati huu ambapo mvua zimeanza, hali inaweza kuwa mbaya zaidi.