Serikali izuie safari za Uingereza na Afrika Kusini haraka

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
Leo tumeamka na taarifa ya kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona huko Uingereza na Afrika Kusini; Kirusi hicho kipya kina uwezo wa kusambaa kwa haraka zaidi ya 70% ya kirusi cha kawaida.

Kufuatia kuibuka kwa aina hiyo mpya ya Kirusi nchi kadhaa zikiongozwa na Ujerumani tayari zimepiga marufuku wasafiri kutoka Uingereza na Afrika Kusini kuingia katika nchi zao

Nalazimika kuishauri Serikali kuzuia haraka wasafiri wote kutoka Afrika Kusini na Uingereza kuingia nchini ili kuiepusha nchi na aina hiyo mpya ya kirusi cha corona
 
Afrika Kusini ni Tanzania na Tanzania ni Afrika Kusini.

Hilo ombi lako litafikiriwa kama asilimia 76 ya watanzania watakufa kwa hicho kirusi kipya.
 
Temana na hicho kirusi mkuu kikija tutapiga maombi ya siku 6 badala ya 3 hadi kirusi kiombe pooh
 
Kama kirusi cha zamani hakikuleta madhara, hicho cha sasa ndio kitaleta maajabu gani?
 
Kije tu,akitaamini kitakavyo shughulikiwa bila huruma kwa mitishamba,nyungu na maombi.
 
Leo tumeamka na taarifa ya kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona huko Uingereza na Afrika Kusini; Kirusi hicho kipya kina uwezo wa kusambaa kwa haraka zaidi ya 70% ya kirusi cha kawaida.

Kufuatia kuibuka kwa aina hiyo mpya ya Kirusi nchi kadhaa zikiongozwa na Ujerumani tayari zimepiga marufuku wasafiri kutoka Uingereza na Afrika Kusini kuingia katika nchi zao

Nalazimika kuishauri Serikali kuzuia haraka wasafiri wote kutoka Afrika Kusini na Uingereza kuingia nchini ili kuiepusha nchi na aina hiyo mpya ya kirusi cha corona
Eh babaake Covid-19 kashatolewa maabara Tena?!🥺
Binadamu tunajimaliza wenyewe kisa mali na uroho wa kuitawala dunia😭
 
Back
Top Bottom