sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Nimeona baada ya video ya watoto wa shule ya msingi wakionekana wakiimba na kucheza nyimbo ya Zuchu serikali imetoka na kuwashusha vyeo walimu wakuu wa shule hizo.
Nimeshangaa sana kwa hatua hii ya serikali maana ni ya kukurupuka na hawajatumia maarifa.
Kwanza naomba niwafahamishe kuwa nyimbo za Zuchu ni kama national anthems kwa watoto wadogo, sio hii Honey tu, karibu zote kuanzia Sukari, Kwikwi nk.
Watoto wanaziimba mstari wa kwanza mpaka wa mwisho ni mpaka Kenya uko. Ipo sababu maana hakuna anaekaa chini akawafundisha nchi nzima watoto kuimba nyimbo za Zuchu. Why only Zuchu? Ni swali la kujiuliza.
Wizara ya elimu inaongozwa na professor ambae pia ndio aliotoa tamko la kushusha vyeo walimu.
Nilitegemea professor baada ya kuona watoto wanacheza na kuimba kwa furaha wimbo huo angefanya critical thinking na kutafuta sababu kwa nini watoto wamevutiwa na huo wimbo ila yeye katika fikra zake aliona suluhu la kuzuia wimbo wa namna hiyo ni kuvua vyeo walimu. Baada ya hapo? Hawezi fikiri zaidi.
Tuna aina hiyo ya maprofesa kwenye nchi yetu wanachoweza ni kuvaa suti na kutishia watu vyeti.
Hakuna professor wa kitanzania aliyegundua formula wala model au falsfa au item ikasaidia watanzania wao wanachoweza ni kukariri vya wenzao kwa level kubwa na kufaulu mitihani.
Nchi za wenzetu kwa sasa wametoka kwenye ufundishaji wa kumezesha watoto. Mwalimu anakaa mbele anaimba aaaa eeee iiii oooo uuuu wenzetu washatoka uko, wapo kwenye learning through play.
Mtoto anajifunza kwa michezo na nyimbo. Darasa linajaa makolokolo ya kuchezea na kuimba mwanzo mwisho madaftari yanaguswa kidogo sana. Sio kama uku katoto ka lower primary unakuta kana begi kuuubwa kanaenda kumezeshwa shuleni spoon feeding ubongo hauchangamki hajifunzi kuadapt mambo mapya.
Nilitegemea professor baada ya kuona watoto wanainjoi wimbo angeanzia hapo kutazama ni namna gani mtaala wetu unaweza ingiza kujifunza kwa kutumia nyimbo zenye maudhui ya Zuchu.
Mnaweza kukaa nae mkapata moja mbili kwanini nyimbo zake ni addictive kwa watoto. Tuna waimbaji wengi ila kwa nini yeye anakubalika na watoto ndivyo watu walioendelea wanavyofanya innovations.
Ubaya wetu waswahili siku zote tunawaza kubomoa badala ya kujenga.
Hakuna mwalimu wala mzazi anaweza mzuia mtoto kuimba nyimbo za Zuchu hakuna. Hawa watoto hakuna anaewafundisha kuziimba mtatafuta watu ubaya bure maana huwezi niambia mtoto wa miaka 2 kafundishwa ni ubongo wake umeweza ku-catch wenyewe.
Wasomi uko serikalini kaeni na Zuchu awasaidie. Kwa sasa mmebadili mtaala ila kama mindset ndio hizi zinazosimamia elimu hakuna kitachobadilika kwenye elimu yetu.
Msipende kujificha kwenye kichaka cha maadili tumieni maarifa. Hamkuwa maprofesa ili mfanye kazi kwa mfumo wa kipolisi.
Weekend njema!