Serikali: Katazo la kutumia Kuni na Mkaa kuanzia Januari 2024 linahusu Taasisi zinazolisha zaidi ya Watu 100 na sio Watu wote

Serikali: Katazo la kutumia Kuni na Mkaa kuanzia Januari 2024 linahusu Taasisi zinazolisha zaidi ya Watu 100 na sio Watu wote

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msemaji mkuu wa Serikal Gerson Msigwa amesema Katazo la kutumia Kuni na Mkaa kuanzia January linahusu Taasisi zinazolisha zaidi ya Watu 100 na siyo Watu wote.

Awali Waziri wa Mazingira Dr Jaffo alisema kuanzia January 2024 itakuwa ni marufuku mtu yoyote kutumia kuni na Mkaa kama nishati ya Kupikia.

Sabato Njema na Mnara wa Babeli
 
Viongozi wa Tanzania ni mbumbumbu sana. Vitu kama hivi vinafanywa kisomi na sio kwa force. Hivi wakikushusha bei ya gas [emoji618]️ ule mtungi mdogo ukawa 12k na unaofuata ukawa 25k kuna mtu atatumia kuni na mkaa???.

Huko vijijini wana uelewa wa kutumia gas?? Wataweza kujaza gas kwa 25k na 57k??. Watu hawawezi kuacha kutumia kuni na mkaa kimasihara hivyo. Tengenezeni misingi mizuri kwanza ili watu waamie wao kwa hiari, shusheni bei za gas
 
Kwakweli yani wanachekesha sana
 
Itachukua miaka mingi sana kufanikiwa kutotumia nishati itokanayo na miti kwaajili ya kupikia na pengine mambo yote.

Heri ingeanzishwa kampeni ya kupanda miti kuliko kukataza matumizi ya kuni ndani ya miezi sita ijayo.
 
Hadi mwakani 99% ya shule za serikali ambazo zinatakiwa kuwekewa hizo infrastructures za kutumia gas huo uwekezaji nina uhakika kwa asilimia 100 utakuwa aujafanyika na si serikali wala private sector mpaka sasa imeagiza vifaa vya kutosheleza taasisi zake tu achilia; binafsi.

Mifumo ya gas ya majumbani inahitaji kukaguliwa na certified engineers, sidhani kama wapo trained wa kutosha nchi nzima mpaka sasa kukagua taasisi za serikali na kufanya gas check at least kila mwaka.

You can go on and on about this; serious it’s ok kuwa na mawaziri vilaza lakini washauri nao kuanzia safu ya katibu mkuu kuwa mambumbu hiyo ni hatari kubwa sana kwa usalama na maendeleo ya nchi.

Yaani huwa ni watu wakujiropokea tu bila ya strategy kwanza ya kufanikisha hiyo sera yao.

Ata kuzungumzia hiyo gharama ya gas yenyewe shida, hao TANESCO wenyewe toka waanze kutumia gas ya TPDC hawajahi lipa ata cent tano na hilo deni juzi serikali imelichukua wao. Halafu ukazilazimishe taasisi kutumia gas bila ya kujiuliza kama wanaweza afford bei au namna watakavyo fund hizo gharama. Kwa mashuleni wazazi wasubiri michango, na kwenye migahawa kupanda kwa bei ya chakula.

Just useless people
 
Kama unapanda miti huku unaendelea kukata miti kwa ajili ya mkaa inakuwa kazi bure tu.
Itachukua miaka mingi sana kufanikiwa kutotumia nishati itokanayo na miti kwaajili ya kupikia na pengine mambo yote.

Heri ingeanzishwa kampeni ya kupanda miti kuliko kukataza matumizi ya kuni ndani ya miezi sita ijayo.
 
Kwa hiyo ndondo la sekondari Sasa litapikwa kwa gas. Laiti viongozi wangekuwa wanawajibika kwa kauli zao sidhani kama kauli hizi zingesemwa
 
Hili swala serikali wala wasihangaike sana.
Wao wawabane wakata miti na wachoma mkaa, kila gunia kodi ipandishwe toka 12000 hadi 60000 kama ushuru na hiyo iwe kwa wilaya moja tu akivuka wilaya nyingine nayo alipe kiasi hicho hicho afu ifumbe masikio
 
Waropokaji katika ubora wao..

Yaani wametuibia fedha zetu,wamekula,wakashiba kurudi nyuma kukumbuka, kumbukumbu zao zikaona jiko la kuni halijawasaidia wao (wametumia gesi na umeme. basi wakasema..

"Huyo masikini asile maana atanenepa kutuzidi".

Hakika kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.

Na asiyefanya kazi za wizi na asile maana mkaa tutakamata - Misemo mipya ya CCM
 
Itachukua miaka mingi sana kufanikiwa kutotumia nishati itokanayo na miti kwaajili ya kupikia na pengine mambo yote.

Heri ingeanzishwa kampeni ya kupanda miti kuliko kukataza matumizi ya kuni ndani ya miezi sita ijayo.
Kama jpm angekuwepo sawa sio huyo bi tozo asiyejua hili wala lile
 
waziri mwenye wizara yake amesema Mwisho wa kutumia mkaa na kuni ifikapo 2025 wananchi hawataruhusiwa kutumia kuni na mkaa , sijajua kila mwananchi watampatia gesi au?

Wanazuia wananchi kutumia mkaa na kuni ili mkaa ukawe kama madawa ya kulevya na wazidi kupata pesa kupitia biashara hiyo ya mkaa na kuni.

(WANAZUIA MKAA NA KUNI , WANASAHAU KUWA WAMERUHUSU MAGOGO NA MBAO)

Naomba kufahamu je? Nikipasua mbao na kutengeneza kuni mtakuja kunikamata?
Serikali mbona inafanya mambo yawe magumu... sema safi mnakitu mtafika mbali. 🙏
 
Gesi itauzwa sh ngapu na kujaza sh ngapi??Wanachezaa
 
Mbao ni miti ya kupandwa.

Mkaa mwingi ni miti pori hukatwa
 
Gesi itauzwa sh ngapu na kujaza sh ngapi??Wanachezaa
Mbezi Beach wameanza tandaza mabomba ya gesi, kuanzia June gesi yakupima, ni wewe ni milioni yako kuunganishiwa mfumo kg 1 1550 ambapo mtungi wa KG 6 utaupata kwa 9300 tu
 
Mkaa ni biashara mbaya na ya hovyo sana kuwahi kubuniwa na binadamu.
 
Back
Top Bottom