Serikali kinashindikana nini kujenga upya na njia 4 kutoka uwanja wa ndege Arusha kwenda mjini?

Doslamari

New Member
Joined
Jun 21, 2024
Posts
4
Reaction score
1,499
Barabara kutoka pale bypass ya East Africa ni ya zamani sana, ni nyembamba, imejaa mashimo, viraka, ukiipata ni sawa tu na njia ya kwenda Kiteto.

Barabara hiyo inatumiwa na watalii hasa wazungu, uwanja wa ndege Arusha una miruko(flights) zaidi ya 150 kwa siku, ni aibu kwa nchi.

Kwanini tusiweze kuficha hii aibu? Ni kwamba nchi yetu ni maskini hivi? Hayo mapato ya utalii kwanini sehemu isitumike kujenga kale ka kipande. Tuna umaskini wa akili kuliko rasilimali. Hv Rais wa nchi anajisikiaje?

Hii nchi inatakiwa ifike mahala Rais anaweza kuondolewa madarakani muda wowote. Unaenda kujenga sports academy kijijini ambayo hahitajiki kisa ni kwao, barabara muhimu sana haijengwi, ni aibu.

Mara ya mwisho ile barabara kujengwa ni miaka ya 90 km siyo 80
 
Ni suala la vipaumbele. Tanzania ni kubwa sana kuliko hicho kipande cha Kisongo unacholilia. Kuna maeneo mengi yanayohitaji fedha zitokanazo na kodi kama elimu, afya, mishahara, ulinzi na ysalama . Hata hiyo Sports academy unayoitaja haijajengwa kwa fedha za walipa kodi. Jiridhishe kwanza na usahihi wa taarifa ndiyo uje uandike.
 
Nadhani uwanja ukikamilika utalete pia mipango mingine mingi mingi!
 
Sasa 2023 mpaka leo , hizo pesa mnapeleka wapi ? Muda huo stendi mpaka leo hamjajenga hapo Arusha .

Wenzenu wanajenga majngo ya luxury hayana muhimu ila wapo fasta nyie kuchelewesha tu kila kitu .
 
Sasa 2023 mpaka leo , hizo pesa mnapeleka wapi ? Muda huo stendi mpaka leo hamjajenga hapo Arusha .

Wenzenu wanajenga majngo ya luxury hayana muhimu ila wapo fasta nyie kuchelewesha tu kila kitu .
2023 ilikuwa usanifu na Mwaka 2024/25 Iko kwenye Bajeti
 
Utekelezaji 2035-2040 sasa hivi tunafanya usanifu kwanza kwa hio endelea kuchomelea soksi
 
Hayati Magufuli aliahidi hii barabara ya njia nne kuanzia TFA complex wakati wa kampeni zake sasa tusubiri porojo kampeni ijayo.
Chatto na sasa Pemba na Unguja zina miundo msingi bora kuliko Arusha
2040 mtakua mmepata barabara za njia 5 sasa hivi chomeleeni soksi kwanza
 
Hii Barabara ilijengwa na EAC, magu aligombana nao sana wajenge njia 4 wakagoma ndo maana walivyomuita aje aizindue nae aligoma kuja
 
Yani Hilo soko hapo kilombero linanuka hatari, naonaga aibu na sijui wale wazungu wanatuonaje kama taifa...ule upande wa kule shopers soko Lina matakataka yananuka haswaaa
 
Mkuu nakuunga mkono. CCM Arusha ina watu wa hovyo mno. Kwa sasa wanakwamishana wao kwa wao. Gambo against wenzake. Siasa za CCM Arusha ni za kipumbavu sana.
 
Arusha Afcon inakuja watu wanajizungusha zungusha tu.

Sasa hivi ilipaswa kuwe na timu ya mpira ligi kuu au moja ya timu za ligi zifanye kituo chake kuhamasisha michezo watu wamekalia siasa tu.
 
Arusha Afcon inakuja watu wanajizungusha zungusha tu.

Sasa hivi ilipaswa kuwe na timu ya mpira ligi kuu au moja ya timu za ligi zifanye kituo chake kuhamasisha michezo watu wamekalia siasa tu.
Siasa pamoja na mambo ya kijinga
 
Arusha Afcon inakuja watu wanajizungusha zungusha tu.

Sasa hivi ilipaswa kuwe na timu ya mpira ligi kuu au moja ya timu za ligi zifanye kituo chake kuhamasisha michezo watu wamekalia siasa tu.
Na jina nalipendekeza kabisa Utalii Sport Club
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…