Barabara za chini zimewashinda za juu wataziweza?
Ni sawa na kutaka kujenga choo kabla ya nyumba
Kupinga barabara za juu DSM ni kupinga maendeleo,huwezi kuwaweka wafanyakazi masaa matatu katika foleni na ukasema unataka uchumi wa nchi ukue,Kujenga barabara za juu ni moja kati ya ufumbuzi wa tatizo lakini kuna haja ya kupanua mji kwa maana ya baadhi ya ofisi na shughuli nyingine kuhamia nje ya mji sio kila kitu Posta na Kariakoo tu.SHIDA YANGU NI JE SERIKALI HII YA ****** ILIYOKOSA UELEKEO INAWEZA KWELI KUJENGA HIZO BARABARA AU NI SIASA NYEPESI TU WANAFANYA?
Tusubili tuone maana jamaa amewakilisha kwa mbwembwe sana.
Mpango huu wa serikali hauna tija na ni ufujaji wa rasilimali ya nchi. Nina uhakika wataalam hawajashauri njia hiyo ya kutatua kero ya foleni.Hebu tusiibeze serikali wakati inapotaka kufanya mambo ya maana. Flyovers Dar ni muhimu na sioni kwa nini mtu atilie shaka kwamba serilkali haitaweza. Tuipe muda serikali ijenge hizi flyovers
Hiyo kwa sasa sahau japokuwa magufuli ni waziri mahiri na mchapakazi na hodari sana kuliko mawaziri wenzake wote na huwa anachokisema ndicho anachokifanya, si mbabaishaji wala mwongo km wenzie na ni waziri anayeaminika kwelikweli ila KWA HILI NAAMINI KUWA KATUDANGANYA LIVE namshauri afute kauli yake itamcost sanaHebu tusiibeze serikali wakati inapotaka kufanya mambo ya maana. Flyovers Dar ni muhimu na sioni kwa nini mtu atilie shaka kwamba serilkali haitaweza. Tuipe muda serikali ijenge hizi flyovers
Siku hizi hata wakuja wote mnamagari, halafu hakuna maendeleo? Mnanshangaza!
Umenena Mkuu!kwanini wasianze na barabara za uchochoro?mfano mbezi goba tangi bovu ambayo itaondoa folen za ubungo kwa wale waendao mwenge,tgt,mikochen etc it wl mean that sio lazima atokae kimara aende ubungo.pia lami itoke mbezi mwisho kwenda airpot.wasisingizie halmashauri kwan hela wanayopewa haitoshi.najua wakitenga kma bilion 40 wanawezafanya la maana.
Swala lingine ni la kujenga nyumba 47/48 Dar na mbili Idodomia. Hivi mandate ya serikali kujenga nyumba haiko chini ya NHC? Kwa nini kila wizara inataka kujenga nyumba zake na sio kutumia shirika la NHC? Je wamegundua nini ambacho NHC hawawezi kufanya? Au ndio danganya toto ile ile ya kukwapua mpunga wa walipa kodi?