Naam,
Siyo busara hata kidogo kuanza kujenga flyovers sasa hivi, labda with exception of TAZARA area. Ujenzi wa barabara mbadala kuelekeza magari mbali na hizo sehemu tete ni muhimu na cheaper zaidi kwa sasa. Ujenzi wa flyovers bado utaendelea kukusanya magari kwenye barabara na intersection hizo hizo na ifahamike kwamba tatizo haliko kwenye hizo intersections peke yake. Magari yakishaondoka kwenye hizo intersections yanarudi kwenye hizo hizo barabara amabzo tayari hazitoshi.
Kwa mfano ukitoka Ubungo kuelkea Morogoro kuna foleni ya kufa mtu siku hizi na wenyeji wanafikiria kuhama. Flyover haisaidii sana katika hilo na matatizo kama hayo yapo Dar nzima. Hakuna ulazima wa kuwa na hiyo shingo ya chupa hapo Ubungo na sehemu nyinginezo.
Solution ipo katika kujenga barabara kuepusha magari kukutana sehemu moja lakini pia kupunguza msongamano kwenye hizo barabara zilizopo sasa. Kwa mfano kulikuwa na proposal ya kujenga ring road kubwa (four, preferably six lane) kuanzia Airport-Kinyerezi, Mbezi mwisho, Bunju. Kisha hii barabara ring road inaunganishwa sasa na barabara ndogo kadhaa zinatoa na kuingiza magari kutoka sehemu kadhaa mjini. Hili likifanyika, traffic jams zitapungua overnight. Cha ajabu wazo hili limeachwa na sasa tunaongelea flyovers!
Ni vyema tukafanya tathmini upya, na bila shaka wazo la flyovers linaweza likawa siyo muafaka kwa sasa.