Mkuu wangeanza na hizi njia tungeona kweli wamedharia kuounguza msongamano!lakini kwa Fly overz lazima Wachekeshe!Lakini si wamezoeaBadala ya kukimbilia hizi flyovers kwa nini wasiimarishe feeder roads? Mfano
Mwananyamala-Sinza
Makongo-Kimara
Wazo-Kibaha
<br />kwanini wasianze na barabara za uchochoro?mfano mbezi goba tangi bovu ambayo itaondoa folen za ubungo kwa wale waendao mwenge,tgt,mikochen etc it wl mean that sio lazima atokae kimara aende ubungo.pia lami itoke mbezi mwisho kwenda airpot.wasisingizie halmashauri kwan hela wanayopewa haitoshi.najua wakitenga kma bilion 40 wanawezafanya la maana.
Hizo fly overs hizo msishangae baada ya muda pot-holes kibao mpaka mnaona magari ya wanaopita chini.......kwi kwi kwi kwi
Siku hizi hata wakuja wote mnamagari, halafu hakuna maendeleo? Mnanshangaza!
<br />Kupinga barabara za juu DSM ni kupinga maendeleo,huwezi kuwaweka wafanyakazi masaa matatu katika foleni na ukasema unataka uchumi wa nchi ukue,Kujenga barabara za juu ni moja kati ya ufumbuzi wa tatizo lakini kuna haja ya kupanua mji kwa maana ya baadhi ya ofisi na shughuli nyingine kuhamia nje ya mji sio kila kitu Posta na Kariakoo tu.SHIDA YANGU NI JE SERIKALI HII YA ****** ILIYOKOSA UELEKEO INAWEZA KWELI KUJENGA HIZO BARABARA AU NI SIASA NYEPESI TU WANAFANYA?
Hii yote ni zile ahadi za Mkubwa za wakati wa Campaing ....sasa anagalia kitu kinacho kuja hapo.......vitu havitafanyika kitaaluma ili tu watu wapate cha kuwaeleza wapiga kura 2015.....hakuna atakaye fikiria juu ya miaka 10 -15 au 20 ijayo....Swali la kwanza la kujiuliza hivi feeder roads zote za Dar zinapitika?......zimejengwa kwa kiwango gani? kujenga Fly overs wakati mipango miji yenyewe issue....Bila ya kufanya maamuzi magumu ya kubomoa badhi ya mitaa... na maeneo mingine ili kuwa na mpango mzuri wa jiji bado ni bure.......!!!! Serekali ilitakiwa kujipanga kwa kuupanga upya mji wa Dar... na sio kukimbilia kujenga Fly overs pekee....take it from me hata baada ya ujenzi wa hizi fly overs katika junction pekee zitawezesha kuhamishia foleni sehemu nyingine tuu kwahiyo foleni bado Dar haitaisha.......
Ujenzi wa fly overs Dar hauepukiki hata kidogo ikiwa ni lazima kumaliza tatizo la foleni. Kenya wanajenga hizo barabara na tayari wameanza kuona matunda yake. Foleni kubwa ziko katikati ya mji kwa sababu ya kushindwa kupishana katika barabara za crossroads; barabara za pembeni nazo ziongezwe mpya na kukarabati zile zilizopo.
Mh.Magufuli amedai bungeni kwamba serikali itaanza ujenzi wa barabara za juu Dar!
Mie Mkweche najiuliza kweli kunahaja ya kujenga barabara za juu wakati barabara nyingi za mitaa ni Mbovu?
kwanini zisijengwe za mitaani kwanza ili kupunguza msongamano maneke ubovu wa barabara za mitaani ni chanzo namba moja cha msongamano dar
Tatizo la Foleni dar es salaam, ni kwenye crossroad kama Mataa ya Ubungo, Mataa ya Magomeni Mapipa, Mataa ya Tazara, Mataa ya Mandela Road, hizi sehemu wakijenga flyover!
Natizo la foleni litakuwa hamna gari zitakuwa zinatembea kwa kasi
Ilikuwa ni Ahadi ya Papo kwa Papo!Sidhani kama mradi flyovers ulikuwemo kwenye budget ya 2010/2011Mkuu wakaya wakati wa kampeni alisema zoezi hili lingeanza mwezi march 2011, now ishakuwa August yan sina hamu na hiyo kitu, sitaki kuamin ktk mradi wao huo!
tumeacha mradi wa mabasi ya kasi tumerukia flyovers. Yote ni mawazo mazuri, utekelezaji ndo kazi. Kabla ya yote waondoe shughuli ambazo zinaweza kufanywa nje ya mji. Mfano mahakama ya kisutu inaweza kuhamia karibu na magereza maeneo ya ukonga ili daktari asisimamishwe asubui kumpisha mahabusu anayeenda kwenye kesi ya kuiba kuku