Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa leo 1, Septemba 2026 kwenye uzinduzi wa Septenba ya Utambulisho
Amesema kuwa,
"Ni kuboresha teknolojia ya kuchapisha vitambulisho. Tumekuwa na maoni mengi kutoka kwa wananchi juu ya uboreshaji wa kitambulisho. Sasa ndugu zangu waandishi wa habari, serikali imeanza kutekeleza uboreshaji wa teknolojia ya uchapishaji wa vitambulisho kutoka teknolojia inayotumia wino hadi teknolojia inayotumia mionzi kuchapisha taarifa katika tabaka (layers) za kitambulisho cha taifa.
Utekelezaji wa uboreshaji huu utawezesha kuongeza ufanisi katika uchapishaji wa vitambulisho vya taifa, kuimarisha uimara na usalama wa taarifa zinazochapishwa kwenye vitambulisho, pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata vitambulisho vya taifa vyenye ubora zaidi na kudumu kwa muda mrefu.
Aitha, utekelezaji wa mpango huu utaenda sambamba na matumizi ya kadi ghafi mpya za vitambulisho vya taifa zenye ubora, uimara na vipengele vya usalama vilivyoboreshwa zaidi ili kuinua ubora wa jumla wa vitambulisho vinavyochapishwa.
Serikali inatarajia kuiwezesha kadi ya kitambulisho cha taifa kubeba taarifa za utambulisho wa mtu zilizopo katika vitambulisho vingine ikiwemo bima ya afya, hati ya kusafiria katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, leseni ya udereva na hivyo kupunguza uwingi wa vitambulisho kwa mwananchi.
Sasa hivi Mtanzania unamkuta kwenye pochi yake ana vitambulisho zaidi ya 20. Tunainza safari ya kupunguza marundo ya vitambulisho kwenye mikoba ya Watanzania."