BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Serikali imesema katika mwaka 2023/2024, shughuli za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2024 zitaendelea.
“Kazi zitakazofanyika ni pamoja na kulifanyia maboresho Daftari la Kudumu la Wapiga Kura; kuboresha mifumo ya menejimenti ya uchaguzi; kuendelea na mchakato wa marekebisho ya sheria za uchaguzi; kuandaa Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani; na kutoa elimu ya Mpiga kura kwa wananchi.
“Nitumie fursa hii kuwaomba viongozi wa vyama vya siasa kuhamasisha wanachama na Watanzania wote wenye sifa kujiandikisha kwenye Daftari hilo na kupata kitambulisho halali cha mpiga kura pale zoezi hilo litakapoanza rasmi,” amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, bungeni leo.