Dodoma: Serikali inatarajiwa kuanza ujenzi wa kiwanda cha mbolea hai katika Kijiji cha Nyamatara, Misungwi, Mkoa wa Mwanza, kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mbolea kwa wakulima wa pamba na hivyo kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.
Hayo yameelezwa na Mhandisi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Tertiano Lyanga, wakati akizungumza tarehe 7/8/2026 katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, ambapo Bodi ya Pamba ni miongoni mwa washiriki.
Lyanga amesema Serikali tayari imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho, ambacho kinatarajiwa kuzalisha mbolea hai kwa kiwango kikubwa ili kukidhi mahitaji ya wakulima wa pamba.
“Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea hai ambacho kitajengwa Misungwi, katika Kijiji cha Nyamatara. Uzalishaji utakapoanza, kitazalisha mbolea kwa kiwango kikubwa ambacho kitamwezesha kila mkulima wa pamba kupata mbolea,” amesema.
Ameeleza kuwa mbolea hiyo hai inatengenezwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana katika mazingira yanayowazunguka wananchi, badala ya kutegemea kwa kiasi kikubwa malighafi za viwandani.
Kwa mujibu wa Lyanga, baadhi ya malighafi zinazoweza kutumika kutengeneza mbolea hiyo ni pamoja na mkaa na samadi ya ng’ombe. Ameongeza kuwa mbolea hiyo imefanyiwa tafiti na imeonesha kufanya vizuri katika uzalishaji wa kilimo.
Mfumo wa kisasa wa ufuatiliaji wa ununuzi wa pamba
Aidha, Lyanga amesema Bodi ya Pamba imeanzisha mfumo mpya wa kisasa unaolenga kupata takwimu sahihi za uzalishaji na ununuzi wa pamba kwa wakati, ambazo hutumika katika kufanya maamuzi na kuchukua hatua stahiki.
“Tumeanzisha mfumo unaoonesha mwenendo wa ununuzi wa pamba. Takwimu hizi ‘live’ zinaonesha kinachoendelea katika masoko yetu ya pamba. Kwa mfano, tangu msimu ulipofunguliwa, pamba iliyonunuliwa kupitia masoko yanayotumia mizani janja ni tani milioni 97, wakati pamba iliyokwisha pelekwa viwandani ni tani milioni 87,” amesema.
Ameongeza kuwa mfumo huo pia umefungwa katika viwanda vya kuchakata pamba ili kuwezesha ufuatiliaji wa idadi ya marobota yanayozalishwa.
Amesema mfumo huo umeonesha kuwa hadi sasa jumla ya marobota 64,000 yameshazalishwa.
“Tunafanya hivyo kuhakikisha tunapata takwimu sahihi za uzalishaji wa pamba na uzalishaji wa marobota kwa kutumia masoko ya kisasa,” amesema.
Kwa mujibu wa Lyanga, upatikanaji wa takwimu sahihi ni muhimu katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya zao la pamba, ikiwemo upatikanaji wa mbegu, viuatilifu na mahitaji mengine muhimu katika uzalishaji.
Amesema takwimu hizo pia husaidia Serikali na wadau wengine kupanga mahitaji ya wakulima na kuchukua hatua kwa wakati, kwa kuwa maamuzi hufanyika kwa kutumia taarifa sahihi na zinazopatikana kwa wakati.