Serikali Kubwa Ni mzigo

Serikali Kubwa Ni mzigo

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nimesikia kuwa serikali ya Tanzania ina mipango ya kupanuka kidogo kuongeza Wizara moja au mbili hivi. Serikali yoyote kubwa sana yenye wizara nyingi huwa siyo mzigo tu kwa nchi, bali pia ni serikali ambayo huwa haina ufanisi kutokana na baadhi ya maeneo ya utendaji kuingiliana. Kipindi cha kwanza cha kikwete kitakumbukwa zaidi kwa kuwa ndicho kilichokuwa na serikali kubwa kuliko yoyote katika historia ya nchi hii tangu Uhuru, na vile vile ndiyo serikali iliyokuwa na utendaji mbovu kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi hii. Sababu kubwa ya Kikwete kuunda serikali kubwa vile ni kwa sababu alikuwa na wanamtandao wengi waliomsaidia kuingia madarakani ambao ilikuwa ni lazima awatafutie viti serikalini. Rais Reagan wa marekani aliwahi kusema kuwa "Government is not a solution to our problem; government is the problem." Kupanua serikali ili kuunda vyeo kwa wafuasi fulani ni kosa sana hasa katika kipindi hiki ambapo dunia nzima inakimbizana na maendeleo kwa spidi ya mwanga.
 
Serikali haina mzigo wala hasara

Ni kazi ya serikali kutoa huduma kwa wananchi

Ikifanikisha hilo kwa gharama yoyote basi hiyo ndio serikali kamili
 
Serikali haina mzigo wala hasara

Ni kazi ya serikali kutoa huduma kwa wananchi

Ikifanikisha hilo kwa gharama yoyote basi hiyo ndio serikali kamili

Nadhani akili yako haina akili.
 
Utitiri wa vyeo..hela yote inaenda kulipa mishahara..posho na usafiri..unategemea kuna maendeleo hapo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom