Serikali kufanya kongamano la kwanza la kodi kitaifa, linalotarajiwa kufanyika Januari 11, 2023 jijini dar es salaam katika ukumbi wa JNICC

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
2,010
Reaction score
4,179



Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeanzisha Kongamano la Kodi Kitaifa litakalowashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Sekta Binafsi ili kajadili namna ya kuboresha Sera za Kodi, kuchochea ukuaji wa uchumi, biashara na uwekezaji nchini.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Sera kutoka wizara hiyo, Bw. Elijah Mwandumbya, katika mkutano na wanahabari ulifanyika jijini Dodoma.

Bw. Mwandumbya alisema Kongamano hilo litarahisisha zoezi la ukusanyaji wa maoni ya wadau kwa ajili ya maboresho mbalimbali ya Sera za Kodi na kuongeza ushirikishwaji wa makundi hayo katika utunzi wa sheria.

“Serikali Kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, ina jukumu la kuratibu upatikanaji wa maoni ya wadau, kuchakata maoni hayo na hatimaye kuyawasilisha kwenye Kamati ya Ushauri wa Kodi, mapendekezo mbalimbali ya sera za kodi yanayotarajiwa kufanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 10(1) cha Kanuni za Bajeti za mwaka 2015”, alibainisha Bw. Mwandumbya.

Alisema katika kongamano hilo litakalokutanisha wataalam wa uchumi, fedha na kodi nchini, mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwa ni pamoja na hali ya uchumi duniani, fursa na athari zake kwenye sera za uchumi, uwekezaji na biashara nchini.

Bw. Mwandumbya aliongeza kuwa mada nyingine zitakazowasilishwa na kujadiliwa ni mfumo wa kodi, ada na tozo mbalimbali pamoja na hali ya ulipaji kodi kwa hiari na changamoto zake katika mazingira ya uchumi, biashara na uwekezaji nchini.

Alibanisha kuwa Kongamano hilo la kipekee pia litajadili mchango wa sekta ya fedha katika kukuza uchumi, biashara na uwekezaji wakati huu wa changamoto za uchumi duniani.

Aidha alitoa rai kwa waalikwa wote wa Kongamano hilo litakalofunguliwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Januari 11, 2023, katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam, kushiriki kikamilifu katika kutoa michango na maoni yao ili kufankisha malengo yaliyokusudiwa.​
 
Safi sana tunazidi kusogea kwenye ustaarabu wa kidunia na hapo maendeleo lazima tutayapata, wananchi tutawaunga mkono na kodi tutalipa kikubwa kodi ya magari muangalie sana hapo.
 
Safi sana tunazidi kusogea kwenye ustaarabu wa kidunia na hapo maendeleo lazima tutayapata, wananchi tutawaunga mkono na kodi tutalipa kikubwa kodi ya magari muangalie sana hapo.
Yote yanawezekana ili hali tutaweza kufikisha hoja husika sehemu husika na wakati husika..Ila tukisalia na kulumbana wenyewe humu jukwaani haitosaidia...Nilazima tuwajibike kuandaa hoja na maswali magumu na kuyafikisha penye utatuzi!
 
Wamualike na Asake wa Tandale
Kwa heshima ipi haswa yeye mwenyewe kujielezea anashindwa sasa huku kwenye mijadala mizito aje kufanya nini?

Alipe kodi kwanza asitafute huruma, Si hua anamajigambo sana sasa anaunyaunya nini...Hapo itakuja kabineti nzito kutoka benki ya Tanzania(BOT) na waziri wa fedha kujibu hoja za msingi kutoka kwa walipakodi na wafanyabiashara tuliona uzalendo na nchi yetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…