Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
PAMOJA na mmiliki wa sasa wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, kampuni ya Acacia Mining, kutangaza kutaka kufunga mgodi wake, serikali ya Tanzania imesema, mgodi huo, uatendelea kufanya kazi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Acacia iliamua kuufunga mgodi wake wa Buzwagi, uliyopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, baada ya kujiridhisha kuwa utajiri wa madini uliyopo katika eneo hilo, umemalizika.
Taarifa ya mgodi huo kuendelea kutumika, imetolewa leo Jumanne, tarehe 19 Januari 2021 na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Prof. Palamagamba Kabudi, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba kati ya serikali ya Tanzania na kampuni ya Madini ya LZ Nickel Limited.
Akizungumza katika halfa hiyo, mbele ya rais John Magufuli, Prof. Kabudi alisema, “faida kubwa ya mradi huu, ni kuanza matumizi mbadala ya miundombinu iliyokuwa inatumika kwenye uendeshwaji wa mgodi wa Buzwagi, ambao unatarajiwa kufungwa hivi karibuni.”
Alisema, muwekezaji huyo mpya, ameomba kwa serikali kuruhusu kutumika kwa miundombinu ya mgodi wa Buzwagi, pindi mgodi huo utakapofungwa.
Aidha, kampuni hiyo imeomba kibali cha kuchenjua masalia ya madini yaliyoko katika mgodi wa Buzwagi, kwa maelezo kuwa teknolojia yake ya kuchenjua masalia hayo kuwa madini, yaweza kufanya kazi hiyo.
Alisema, “…mheshimiwa rais, wawekezaji hawa wameomba mgodi huu utakapofungwa wauchukue ili badala ya kufungwa ufanye kazi nyingine, ili kuuongezea uhai zaidi sababu wanasema yale masalia yaliyoko pale Buzwagi bado yana madini.”
Ameongeza, “…na kwa teknolojia hii mpya, bado watavuna madini haya ambayo sasa ni rundo. Teknolojia ya wale ilikuwa haiwezi kuyachenjua. Hawa wanaweza; sasa masalia yote ya Buzwagi yatarudishwa tena kwenye mitambo na kutoa madini.”
Prof. Kabudi alitoa taarifa hiyo wakati anataja faida za mkataba huo wa uchimbaji madini ya Nickel katika mgodi wa Kabanga mkoani Kagera na ujenzi wa Kiwanda uchakataji madini mkoani Shinyanga.
Ametaja faida nyingine za mradi huo, ni kuongezeka kwa ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya madini.
“Mradi huu utaongeza ukuaji wa sekta ya madini, kwa kuanzisha na kuendeleza uchimbaji wa madini ya Nickel na madini muambata kama kopa na kobati,” ameeleza