Serikali kufufua mgodi wa Buzwagi uliofungwa na Acacia kwa madai ya Madini kuisha Ardhini

Huko Tulawaka pamoja na kuachiwa karibia kila kitu na beberu, he STAMIGOLD, wametengeneza faida kiasi gani??

Wangeruhusu tu wachimbaji wadogo wahangaike huko, serikali ikusanye mapato.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Na ndio hizo hizo zinawapa ruzuku. Kuweni na shukrani basi? Bila CCM kuwepo sijui nyie wengine mngekuwa wapi?
 

Moja kati ya parameters zinazotumika kutambua cut-off grade ya mgodi ni gharama za method inayotumika.. Cut-off grade inatofautiana kulingana na utofauti wa method inayotumika.

Binafsi bado sioni sababu ya kupinga kama muwekezaji amehakikisha anayo mbinu itakayomfanya apate faida. Cha msingi sheria zote zifuatwe.
 
Na ndio hizo hizo zinawapa ruzuku. Kuweni na shukrani basi? Bila CCM kuwepo sijui nyie wengine mngekuwa wapi?
Acha kutudanganya,vipi sehemu nyingine za dunia ambapo hamna huyo mnyama wa kijani,Maisha si bora zaidi.
 
Acha kutudanganya,vipi sehemu nyingine za dunia ambapo hamna huyo mnyama wa kijani,Maisha si bora zaidi.
Majungu hayo, hama nchi kwani lazima uishi Tanzania? UK wana vyama viwili tu vikubwa na wanabadilishana USA vile vile wana vyama vikubwa viwili tu na ndio vinabadilishana. Mlizoea enzi zenu chuma kiko Ikulu sasa wacha kiwasafishe. Una haki ya kuhamia Bengal!
 
Unatuumiza macho na marangi yako ya kusisitiza unayo amini wewe.
 

Nakubaliana na wewe kwenye hilo suala la cut grade na njia ya uchimbaji na processing. (Upo sahihi kabisa)

Pia mimi sijapinga muwekezaji kuendeleza uchimbaji.

Wasi wasi wangu tu ni njia ambayo itatumika na kuzalisha faida. Hapa ndio nina mashaka.
 
Hakuna muwekezaji anataka kufanya KAZI YA HASARA. Kama vile ambavyo biashara binafsi zinafungwa nyingi, migodi nayo inafungwa sababu hakuna faida. Sirikali angalieni kodi zenu na regulations zenu. Watz ndio wataumia mwisho wa siku.
 

..maelezo yako ni ya uongo.

..na hata yangekuwa ya ukweli hayaisafishi barrick kutokana na wizi wa madini hapa Tz.

..sisi tulisema tunadai usd 191 billion lakini bila maelezo ya kutosha tumekubali kishika uchumba cha usd 300 million.

..mimi nadhani kuna MAJIZI ndani ya ccm na serikali ndiyo yameingia makubaliano ya kifisadi ya kukubali kishika uchumba toka barrick.
 
Kichwa cha habari na taarifa haviendani, huyu muwekezaji haendi kuchimba madini bali anataka kuchenjua zile shehena za makinikia na udongo uliojazwa kule TSF na zile low grade ambazo Acacia wameziacha kuepuka gharama ya kuendesha uchenjuaji wa hasara kutokana na kiasi cha madini wanayotegemewa kuyapata kutoka kwenye mchanga huo.

Pia ikumbukwe kwamba Buzwagi madini hayajaisha, bali gharama zinazohitajika kuyachimba madini hayo ni kubwa sana hivyo kupelekea mgodi kujiendesha either kwa faida ndogo sana ama kwa hasara.

Inasemekana (hili sina uhakika nalo), kampuni iliyofanya utafiti wa madini pale Buzwagi nadhani ni Pangea minerals, waliwaingiza chaka ABG na kuwafanya watengeneze Mining map yao nje ya eneo lenye kiasi kikubwa cha madini, hali hii ilipelekea kubadili ramani yao ghafla sana kuelekea upande uliokua na kambi za kampuni ya ulipuaji, na hivyo kupelekea shimo kubana.
Inasemekana iliwalazimu kuanza uchimbaji upya ili wapanue shimo hilo, kitu ambacho walikitafsiri kama hasara kwao.
 
Porojo tu.

Kutumia mabanda yalioachwa kama madarasa, soko ama makazi ndiyo kufufua mgodi??

Rubbish!!!
Kampuni kama yapi markez ikimaliza mkataba wa ujenzi wakaacha kambi yao mikononi mwa serikali, na wananchi wa eneo hilo wakaamua kuitumia kufungua shule ya sekondari au chuo cha ufundi kuna ubaya gani?
Wakati mwingine makamanda sijui huwa mnatumia nini kufikiri?! Mnaiabisha sana chadema. Chadema iliyokuwa hazina ya hoja mbadala sasa hivi imegeuka kuwa genge la wasemaovyo tu. Bure kabisa 😢😢
 
Alafu mwisho wa siku inagundulika mmiliki wa huu mgodi ni kagame wakiwa na share na magufuli nyuma ya pazia.
 
Ulikuwa ni utani tu, ulikosea baada ya neno kufika ukaandika kufila cutoff.....
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]nikasema sasa huyu jamaa ni mtu asiyejulikana. Ngoja nishike adabu zangu tu[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Hoja ya Kabudi ni ya kipuuzi kabisa. Inawafaa wajinga wa sekta hii.

Wanachotaka kufanya hiyo kampuni nyingine ni sawa na ukawa na shamba la mahindi, unavuna kutumia combine harvester. Umemaliza, halafu anakuja mtu anaomba apite kwenye shamba lililovunwa kuangalia uwezekano wa kuvuna mahindi yale machache yaliyokuwa yameanguka kabla ya harvester kupita ili aokoteze na kujipatia riziki ndogo.

Hiyo teknolojia anayoiongela Kabudi imekuwepo kwa miaka mingi. Mineralization inafuata structure. Na kuna wakati kunakuwa na minor structural displays kama vile fractures na shear displays ambako mineralized fluids zilipenya wakati wa mineralization. Hizi hazifuatwi na makampuni makubwa ya uchimbaji. Vikampuni vidogo huweza kuyachukua mawe, kisha kufanya crushing ili kupata aggregates ambazo baadaye zinapita kwenye sorting systems ambapo zile zilizokuwa mineralized zinakuwa picked na kwenda kufanyiwa processing kwaajili ya kupata madini yanayotafutwa.

Kwa ujumla, unachokipata kupitia process hiyo ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na kile alichokipata mvunaji wa kwanza. Hiyo ndiyo sababu huwezi kuona kampuni kubwa zikijishughulisha na uvunaji dhahabu wa namna hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…