Serikali kufunga mipaka kwa upungufu wa chakula ni kuwaua wakulima

Serikali kufunga mipaka kwa upungufu wa chakula ni kuwaua wakulima

fisi 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
3,280
Reaction score
4,645
Ni kweli ina nia ya kusaidia janga la njaa. Lakini kwa nini kila wakati wa kuuza bei ya chini ni wakulima tuu.

Kwanini bidhaa nyigne hatua kama hizi hazichukuliwi. Sisi tunaotoa muda wetu kulima na kudharaulika tunalazimishwa kulisha watu wavivu na wengine wanaotukashifu tunapoingia shambani kupambana.

Serikali hiyo hiyo haitoi msaada wowote kwetu wakulima. Kidogo wanachotoa kina masharti magumu na mara nyignine kinaliwa juu kwa juu mpaka kitufikie ni robo.

Serikali sasa iache wakulima nao tufaidi mabei makubwa hata laki tano kwa gunia la mahindi poa tuu. Kila mmoja ale urefu wa kamba yake.
 
Mtu pekee mnyonge kuliko raia wote nchi hii ni mkulima. Bei ya mafuta au pembejeo ikipanda muathirika mkuu ni mkulima. Ikitokea neema ya bei ya chakula kidogo tu serikali inaingilia kati. Lengo ni kumfanya aendelee kubaki mnyonge daima.[emoji34][emoji34][emoji34]
 
Huu mwaka mvua haziku nyesha nyingi hata mikoa ambayo ilikuwa inapata mvua nyingi kuanzia mwisho mwaka jana mpaka leo mvua haziku nyesha sana so serikali kuzuia kuuzwa nje chakula wapo sawa cha msingi wakae chini na wakulima wapangiane bei ambazo hazito muumiza mkulima wala mlaji.
 
Ni kweli ina nia ya kusaidia janga la njaa. Lakini kwa nini kila wakati wa kuuza bei ya chini ni wakulima tuu. Kwa nini bidhaa nyigne hatua kama hizi hazichukuliwi. Sisi tunaotoa muda wetu kulima na kudharaulika tunalazimishwa kulisha watu wavivu na wengine wanaotukashifu tunapoingia shambani kupambana. Serikali hiyo hiyo haitoi msaada wowote kwetu wakulima. Kidogo wanachotoa kina masharti magumu na mara nyignine kinaliwa juu kwa juu mpaka kitufikie ni robo. Serikali sasa iache wakulima nao tufaidi mabei makubwa hata laki tano kwa gunia la mahindi poa tuu. Kila mmoja ale urefu wa kamba yake.
Unataka yatokee ya Sri Lanka nin mkuu..
 
Naunga mkono hoja.
Dawa ya food security sio kuzuia chakula kuuzwa kwenye soko zuri nje ya mipaka. Ila ni kutoa bei nzuri ya mazao Hayo ndani.
 
Tulisema hapa muda mrefu mavuno sio mengi na wanastuka muda huu mazao yashaisha kitambo
 
wazuie tu kg 20 ya unga nimenunua jana 25000 elfu Debe moja elfu 17 na niko mikoa ya wakulima,,mpaka mwezi wa 12 itakuwaje
 
Km una family extended lzm Bei ikuchome ila km single au mko wawili ndani fresh febe likiwa 20000
 
Back
Top Bottom