Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Serikali ya Uganda imeingia mkataba na Kampuni ya Teknolojia ya Global Systems LLC ili kuweka vifaa vya kielektroniki (tracking devices) kwenye vyombo vyote vya usafiri nchini humo.
Waziri wa Usalama wa nchi hiyo, Meja Jenerali Mstaafu Jim Muhwezi amethibitisha jana kuwa wamesaini mkataba wa miaka 10 na kampuni hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila chombo cha usafiri kinakuwa na kifaa cha kielektroniki kinachoonesha mwenendo wa chombo hicho ili serikali iweze kuchukua hatua za haraka panapotokea dharura yoyote.
Waziri huyo amebainisha kuwa mkataba huo umesainiwa kwa siri na hauwezi kujadiliwa na umma. Kampuni hiyo itafanya kazi chini ya usimamizi wa serikali ya Uganda kwa muda wa miaka 10, kisha itatoa teknolojia hiyo kwa serikali. Wamiliki wa vyombo vya usafiri watalazimika kulipa Shilingi 20,000 za Uganda (sawa na Tsh. 13,000) kwa mwaka.
Mkataba huo kwa sasa unasubiri kuthibitishwa na serikali. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aliwahi kudokeza kuhusu kuweka vifaa vya kielektroniki kufuatilia nyendo za vyombo vya usafiri wakati alipolihutubia bunge mwaka 2018 wakati taifa hilo lilipokuwa katika wimbi la kuuawa kwa wanasiasa, viongozi wa kidini na maafisa usalama.
Tangu wakati huo, taifa hilo limeshuhudia kuuawa kwa Mbunge wa jimbo la Arua, Ibrahim Abiriga, Kamanda wa zamani Polisi wa Wilaya ya Buyede na Msemaji wa Polisi ambao wote waliuawa na watu waliokuwa kwenye pikipiki. Tukio la hivi karibuni zaidi ni la kunusurika kuuawa kwa Waziri wa Kazi, Jenerali Katumba Wamala, ambapo wauaji walifanikiwa kumuua binti yake, Brenda Nantongo na dereva wake, tukio lililofanyika saa tatu asubuhi.
Zaidi, serikali inakusudia kufunga kamera za usalama (CCTV) na kuongeza kikosi cha usalama. Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa vikali na watetezi wa haki za binadamu, wakiwamo Chama cha Wanasheria Uganda (ULS), wakidai kuwa serikali inakiuka haki ya faragha ambayo inatambuliwa kikatiba.
“Kila Mganda ana haki ya kikatiba ya faragha. Maamuzi kama haya yalipaswa kufanyika kwa njia ya uwazi. Mara zote, Bunge linapaswa kushirikishwa linapokuja suala la Kikatiba,” alisema Pheona Nabasa Wall, Rais wa ULS.