Serikali kuja na kifurushi cha gesi ya kupikia cha Sh 500 au 1,000 ili Mtanzania anunue gesi badala ya mkaa na kuni

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Suleiman Jafo amelitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mkaa mbadala unaotokana na makaa ya mawe ili kuokoa mazingira.

Soma hapo kwa umakini ili upate kujua ni mkaa wa namna gani unazungumziwa hapo.

Na lengo la kutumia huo mkaa mbadala na kifurushi cha gesi ya kupikia ni ili kuokoa mazingira yetu.
Hadithi na porojo za mkaa mbadala zilianza miaka ya 70 enzi za Nyerere wakati Stamiko iko kileleni.
 
Katika kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia, serikali yetu itakuja na utaratibu wa kumruhusu mteja kuinunua gesi kwa bei ndogo kulingana na mahitaji yake.

Kwa sasa wengi wanashindwa kumudu kutokana na gharama kubwa zilizopo, hivyo mchakato wa kuzipunguza unaelekea mwishoni ili kulifanyia mapinduzi suala hilo.

Moja ya vikwazo kwa Watanzania kutumia gesi ni kwamba lazima uwe na fedha nyingi kwa mkupuo. Teknolojia inayoruhusu mtu kununua gesi ya Sh500 au Sh 1,000 ipo na inamwezesha mtu kununua gesi kama anavyonunua kopo la mkaa au fungu la kuni.

Kwa sasa gesi inayouzwa kwa mtungi wa kuanzia kilo sita, ni wastani wa Sh25,000 hivyo kuwa juu ya mahitaji ya baadhi ya wanaohitaji kiasi kidogo kwa matumizi yao au wasio na uwezo wa kifedha kumudu bei ya mtungi huo.

Teknolojia hiyo itakuwa mkombozi kwa Watanzania na itapunguza matumizi ya kuni na mkaa kupikia hasa kwa wananchi wa vijijini. Mazingira yetu yanafanana na India kwa kiasi kikubwa lakini wao asilimia 98 wanapika kwa kutumia gesi.

Kiuhalisia bei ya gesi ni rahisi kuliko mkaa na kuni, lakini wananchi wamezoea kununua kuni na mkaa katika vipande vidogovidogo ndio maana haionekani kuwaumiza wengi hivyo gesi inahitaji ubunifu wa kibiashara ili kuendana na uwezo na mahitaji ya Watanzania.

Chanzo: Mwananchi

Ahsanteni
Teknolojia hii tunayo M-Gas tayari.
Karibu M-Gas ujipatie kifurushi cha gesi cha kuanzia Tsh 1000.

Call/WhatsApp 0747744895
View attachment 2389441View attachment 2389442

Tutunze mistu na miti yetu kwa kuchagua kupikia M-Gas.
Nafikiri ningekuwa mimi Serikali ningehamasisha Watanzania waweze zalisha Na Kupikia BIOGAS unayoweza patikana toka mabaki ya vyakula- hili ndo suluisho la kudumu. Buku kwa mtanzania wa kijijini is not a joke
 
Bado haisaidii kitu, kwa maana kila akipika atajikuta ananunua gesi. Nani yupo tayari kununua gesi ya 2000 ambayo atapikia ndani ya nusu saa tu imeisha
Mbona kuni na mkaa huwa tunanunua na tunapikia baada ya hapo tunanunua tena boss. Karibu M-Gas boss. Piga namba 0747744895 upate kuhudumiwa mapema.
Screenshot_20221017_063748.jpg

images (19).jpeg
images (21).jpeg

mmexport1664713103754.jpg
 
Serikali ina mipango mingi Sana isiyokuwa na cohesion..

STAMICO na Jafo wanasema wamegindua mkaa rafiki wa mazingira serikali haifanyi kitu..

Makamba anasema anazindua gas ya kupima.sasa kipi hasa ni uelekeo wa serikali?
yani kiufup Tanzania kama mnala wa baber wao kwa wao lugha znaenda tofaut ss
 
Nafikiri ningekuwa mimi Serikali ningehamasisha Watanzania waweze zalisha Na Kupikia BIOGAS unayoweza patikana toka mabaki ya vyakula- hili ndo suluisho la kudumu. Buku kwa mtanzania wa kijijini is not a joke
Hii ndio habar ya mjini
Sema serikali ina mambo yake kwenye hizo gas nyingine
 
Katika kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia, serikali yetu itakuja na utaratibu wa kumruhusu mteja kuinunua gesi kwa bei ndogo kulingana na mahitaji yake.

Kwa sasa wengi wanashindwa kumudu kutokana na gharama kubwa zilizopo, hivyo mchakato wa kuzipunguza unaelekea mwishoni ili kulifanyia mapinduzi suala hilo.

Moja ya vikwazo kwa Watanzania kutumia gesi ni kwamba lazima uwe na fedha nyingi kwa mkupuo. Teknolojia inayoruhusu mtu kununua gesi ya Sh500 au Sh 1,000 ipo na inamwezesha mtu kununua gesi kama anavyonunua kopo la mkaa au fungu la kuni.

Kwa sasa gesi inayouzwa kwa mtungi wa kuanzia kilo sita, ni wastani wa Sh25,000 hivyo kuwa juu ya mahitaji ya baadhi ya wanaohitaji kiasi kidogo kwa matumizi yao au wasio na uwezo wa kifedha kumudu bei ya mtungi huo.

Teknolojia hiyo itakuwa mkombozi kwa Watanzania na itapunguza matumizi ya kuni na mkaa kupikia hasa kwa wananchi wa vijijini. Mazingira yetu yanafanana na India kwa kiasi kikubwa lakini wao asilimia 98 wanapika kwa kutumia gesi.

Kiuhalisia bei ya gesi ni rahisi kuliko mkaa na kuni, lakini wananchi wamezoea kununua kuni na mkaa katika vipande vidogovidogo ndio maana haionekani kuwaumiza wengi hivyo gesi inahitaji ubunifu wa kibiashara ili kuendana na uwezo na mahitaji ya Watanzania.

Chanzo: Mwananchi

Ahsanteni
Teknolojia hii tunayo M-Gas tayari.
Karibu M-Gas ujipatie kifurushi cha gesi cha kuanzia Tsh 1000.

Call/WhatsApp 0747744895
View attachment 2389441View attachment 2389442

Tutunze mistu na miti yetu kwa kuchagua kupikia M-Gas.
Sasa mkuu si vilevile wanachofanya m gas aka kopa gas
 
Back
Top Bottom