Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Serikali ya Tanzania inajenga Hospitali mpya ya Rufaa wilayani Ukerewe mkoani Mwanza katika jitihada za kutokomeza vifo vya mama na mtoto vinavyotokea baada ya kukosa huduma za matibabu ya kibingwa.
Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu wakati akikagua eneo la ujenzi huo, akisema hospitali hiyo itajengwa katika kijiji cha Bulamba kata ya Bukindo na tayari bilioni nne zimeshatengwa kwaajili ya kuanza utekelezaji wake.
“Hospital hii itakuwa na uwezo wa kutoa huduma nne za matibabu ya kibingwa, kama vile upasuaji, upasuaji wa mifupa, magonjwa ya wanawake na uzazi pamoja na magonjwa ya watoto." amesema Waziri Ummy Mwalimu
Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Elkana Balandya, amesema kukamilika kwa hospitali hiyo mpya ya rufaa Mkoa kutasaidia kutoa matibabu ya kibingwa kwa wananchi hata nyakati za usiku.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi, amewataka wakazi wa kijiji hicho itakapojengwa hospital hiyo kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika ujenzi wa hospitali mpya ya Mkoa ya Rufaa wilayani humo kwa kulinda vifaa vya ujenzi wake.
Naye Mkuu wa wilaya hiyo Hassan Bomboko amemshukuru na kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa hospital hiyo ambayo amesema itatoa matibabu ya kibingwa kwa wakazi wa kisiwa hicho na kuondoa usumbufu wa kufuata matibabu ya kibingwa mkoani Mwanza.