Serikali Kujenga Kituo cha Forodha Kakozi, Momba

Serikali Kujenga Kituo cha Forodha Kakozi, Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

SERIKALI KUJENGA KITUO CHA FORODHA KAKOZI, MOMBA

"Je, kuna mpango gani wa kuweka kituo cha forodha Kakozi, Momba ili kuunga mkono jitihada za kujenga Soko la Mazao la Kimataifa?" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania ina utaratibu wa kupitia na kufanya tathmini sehemu zote zinaweza kujengwa Ofisi kwaajili ya ukusanyaji kodi. Utaratibu unazingatia uwiano wa gharama za ukusanyaji wa mapato na kiwango cha kodi kinachotarajiwa kukusanywa pindi Ofisi zitakapofunguliwa kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi katika eneo husika" - Mhe. Hamad Chande, Naibu Waziri wa Fedha

"Serikali inaendelea kufanya tathmini ya kina katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kakozi, Momba na mipaka mbalimbali hapa nchini. Maeneo yatakayokidhi vigezo vya kujenga Ofisi za forodha kulingana na tathmini hizo taratibu za uanzishwaji wa Ofisi zitaanza kwa kuzingatia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha" - Mhe. Hamad Chande, Naibu Waziri wa Fedha

"Julai 2021 Waziri wa Fedha na Mipango alifanya ziara na kutembelea kituo cha forodha. Majibu ya Serikali yanasema kwamba wanafanya tathmini kwa kina. Je, Tathmini ya kina inachukua muda gani kukamilika" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Kutokana na umuhimu wa kituo cha forodha cha Tunduma (kimebeba nchi nyingi za SADC) na kituo kuonekana kuzidiwa kutoa huduma za forodha. Je, Serikali haioni kuna haja na uharaka sana wa kuongeza kituo cha forodha Kakozi ili kunusuru mapato yanayopotea na kuongeza pato kwa Taifa" - Mhe. Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba

"Tathmini itakamilika ndani ya mwaka wa fedha 2023-2024. Namuelekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aangalie uharaka wa ujenzi wa kituo cha forodha Kakozi, Momba endapo atajiridhisha kutokana na tathmini yake" - Mhe. Hamad Chande, Naibu Waziri wa Fedha
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-11-01 at 11.32.11.mp4
    22.5 MB
  • WhatsApp Image 2023-11-01 at 11.33.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-01 at 11.33.13.jpeg
    348.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom