Serikali Kujenga Masoko Matano ya Mazao Halmashauri ya Songea

Serikali Kujenga Masoko Matano ya Mazao Halmashauri ya Songea

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WAZIRI JENISTA MHAGAMA ASEMA SERIKALI KUJENGA MASOKO MATANO YA MAZAO HALMASHAURI YA SONGEA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho awaomba wananchi kuchangamkia fursa za uchumi zitakazo chochewa na ujenzi wa Masoko ya Mazao yanayotarajiwa kujengwa na Halmashauri ya wilaya ya Songea.

Juhudi hizo za serikali zitakuza uchumi kwa wananchi na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato kwa serikali.

Wito huo umetolewa katika ziara yake ya kutembelea na kujionea miradi ya maendeleo katika Jimbo la Peramiho Halmashauri ya wilaya ya Songea wakati akizungumza na wananchi katika matukio tofauti katika kata mbili za Mbingamwalule na Peramiho tarehe 18/07/2023.

“Tumepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa masoko ya mazao tutajenga soko kubwa Peramiho; Tutajenga Mpitimbi, tutajenga Matimila, tutajenga Mbingamwalule, na tutajenga katika kijiji cha Muhukuru" - Mhe. Jenista Mhagama

Alifafanua kwamba Ujenzi wa Miundo mbinu ya barabara ya Lami kuanzia kata ya Mbingamwalule inayoenda mpaka Kizuka ni ufunguzi wa Uchumi kutoka Mpaka wa Tanzania na Msumbiji na utasaidia kutoa mazao shambani kwenda kwenye masoko ya mazao.

Waziri Mhagama amesema, serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepanga kuunganisha kituo cha mabasi kitakachojengwa kata ya Mbingamwalule ili kusaidia wageni kupata urahisi wa kufika kwenye soko la mazao lilopo kwenye kata hiyo, na hivyo kufungua fursa mbalimbali za uchumi.

Akizungumzia kuhusu Mradi wa soko la kisasa uchuuzi wa mahitaji madogo madogo ya nyumbani lilojengwa kijiji cha Peremiho “A” ujenzi uliotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) amesema nimefurahi kuona wafanyabiashara wanafanya shughuli zao katika eneo zuri na bora la kibiashara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mhe. Menas Komba amesema ujenzi wa soko la mazao katika kijiji cha Matomondo kata Mbingamwalule Halmashauri ilipokea jumla ya shilingi milioni 198 ambayo inatekeleza mradi na ujenzi unaendelea.

“Tunataka kukamilisha ujenzi wa vyoo ili tuwalete wachuuzi waliopo mtaani kwenye soko, waanze kuzoea kutumia soko jipya la mazao wakati tukimalizia ujenzi kwenye baadhi ya maeneo ya soko,” alisema.
 

Attachments

  • F1ZWZmHXgAE11Tn.jpg
    F1ZWZmHXgAE11Tn.jpg
    164.7 KB · Views: 10
  • F1ZWaNkXsAAletH.jpg
    F1ZWaNkXsAAletH.jpg
    148.1 KB · Views: 7
  • F1ZX_NEWAAIdnvw.jpg
    F1ZX_NEWAAIdnvw.jpg
    119.1 KB · Views: 8
  • F1ZX_4rXwAAG7-x.jpg
    F1ZX_4rXwAAG7-x.jpg
    105.8 KB · Views: 8
Back
Top Bottom