Tetesi: Serikali kujenga shule za vipaji kila mkoa

Tetesi: Serikali kujenga shule za vipaji kila mkoa

Inasemekana kuwa serikali inaweza kuwa na mpango wa kuzirudisha shule za vipaji maalumu hasa kwa kuboresha zile zilizopo na kujenga nyingine kila mkoa ili kulinda na kukuza vipaji vya watoto wa kitanzania bila kujali vipato vya familia wanazo toka.

Shule hizo ambazo zitakuwa kwa kila kanda kwa Alevel na kila mkoa kwa Olevel zitachukua watoto walifanya vizuri kutoka shule za Olevel na msingi kama zilivyo kuwa hapo awali shule za ilboru ,mzumbe, Msalato etc.

Mpango huo utagusa kozi zote na combination zote hapa nchini na zitatuhusu hata vijana kutoka nchi za jirani kujiunga kwa ada kubwa au kwa ufadhili za serikali zao.

Mpango huo pia utaenda sambamba na kuandaa vyuo maalumu vya elimu ya juu kwa vijana wanao fanya vizuri ili kujenga uzalendo na kupata vijana wazuri watakao chukua majukumu makubwa hapa nchini.

Pamoja na hilo pia kuna uwezekano wa kufufua chuo cha siasa ambapo hakuna mtu atakaye gombea urais au ubunge bila kupitia chuo hicho ambacho kitajikita kwenye utawala, Katiba, uongozi, Mambo ya nje, Siasa na mambo yanayo ihusu Tanzania kwani kumebainika wengi wanaogombea ubunge hata urais hawaijui vizuri nchi yao.

kwa heri...

May be it was about time.
Kuhusu chuo cha siasa, nasita. Tumewahi kuwa na Kivukoni na waliopitia hapo ndio wametufikisha tulipo. Siasa unazaliwa na mlengo au huna. Kujua nchi yako ni elimu ya uraia (civics na historia). Mshikamano - rudisheni Jeshi la kujenga taifa kama requirement baada ya form 6.
 
Tatizo la JKT hakuna mtaala mzuri wa kizalendo zaidi ya kupeana adhabu ngumu na za mateso au kukomoana.
 
Kila kukicha kujenga uwezo kujenga, shule kujenga, barabara kujenga, ofisi kujenga, polisi kujenga, mahakama kujenga, reli kujenga, maji kujenga, akili yetu ka ya fundi seremala kila tatizo gonga msumari
 
Litakuwa jambo la busara sana wasiishie hapo tu wanafunzi 100 wenye ufaulu mzuri wapelekwe nje kwenye vyuo bora.
 
Kila kukicha kujenga uwezo kujenga, shule kujenga, barabara kujenga, ofisi kujenga, polisi kujenga, mahakama kujenga, reli kujenga, maji kujenga, akili yetu ka ya fundi seremala kila tatizo gonga msumari
ujenzi wa miundo mbinu ndio maendeleo
 
Tatizo la JKT hakuna mtaala mzuri wa kizalendo zaidi ya kupeana adhabu ngumu na za mateso au kukomoana.
Kupeana adhabu ngumu, mateso na kukomoana - hayo yanaweza kurekebishwa na sheria au revised JKT regulations. Muulize saikolojia yeyote aukueleze mshikamano wa watu walioshiriki shida (percieved or real).
 
ujenzi wa miundo mbinu ndio maendeleo
sio kweli, tunatakiwa tujenge fikra za watu kwanza bila hivyo hamna tunachofanya, ndio maana tunajenga madaraja ya watembea kwa miguu watu wanajisaidia, huku kote kunatokana na watu kutokujengwa ki fikra.
 
Jenga miundo mbinu simamia sheria, Jenga shule watu wakasome, wakati wanasoma simamia sheria otherwise watageuza madarasa kuwa vyoo.

Elimu ni pamoja na kusimamia sheria,
 
Ndarichako umefikia wapi na huu mpango?
 
Back
Top Bottom