PreGE2025 Serikali Kulipa fidia ya Shilingi Bilioni 6 kwa wananchi wapisha ujenzi wa Kiwanja wa Ndege Kilwa Masoko

PreGE2025 Serikali Kulipa fidia ya Shilingi Bilioni 6 kwa wananchi wapisha ujenzi wa Kiwanja wa Ndege Kilwa Masoko

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Serikali imeahidi kulipa madai ya fidia ya shilingi bilioni sita kwa wananchi waliotoa maeneo yao ili kupisha ujenzi wa Kiwanja wa Ndege Kilwa Masoko mkoani Lindi kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba kwa njia ya simu wakati Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Amos Makalla akiwa kwenye mkutano wa hadhara wilayani Kilwa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Awali, wananchi hao walimweleza Makalla uwepo wa madai hayo baada ya kupisha ujenzi wa kiwanja hicho cha ndege, ambapo waliiomba Serikali kuwalipa fidia hiyo ili wakanunue maeneo mengine.

 
Back
Top Bottom