Serikali: Kuna kundi kubwa la watoto wenye jinsia mbili, lakini wanafichwa na wazazi na kushindwa kupatiwa matibabu

Serikali: Kuna kundi kubwa la watoto wenye jinsia mbili, lakini wanafichwa na wazazi na kushindwa kupatiwa matibabu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), imesema kuna kundi kubwa la watoto wenye jinsia mbili, lakini wanafichwa na wazazi, hivyo kushindwa kupatiwa matibabu.

Kutokana na hatua hiyo, jamii imetakiwa kuacha imani potofu na kutumia fursa zilizopo katika mamlaka hiyo, ili watoto hao wafanyiwe uchunguzi kubaini jinsia yenye nguvu na kujengewa uwezo.

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimatafa (DITF), yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Udhibiti anayesimamia uingizaji, usambazaji na matumizi ya kemikali nchini, Daniel Ndiyo, alisema kundi kubwa la watoto wenye jinsia linafichwa.

“Mamlaka kwa kushirikiana na madaktari mbalimbali nchini, inafanya uchunguzi kwa watoto wanaozaliwa na jinsi mbili tofauti, lengo ni kuangalia ipi ina nguvu na inaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,”alisema. Alisema wakati umefika jamii kuacha kuwaficha watoto hao na kuwapeleka katika mamlaka ya mkemia mkuu ili kufanyiwa uchunguzi.

Ndiyo alisema watoto wanaozaliwa na jinsi mbili tofauti wapo na wamebaini wanafichwa, hivyo ni vyema wananchi kujengewa uwezo wa elimu na kubaini kuwa hilo ni tatizo la kawaida hivyo waache imani potofu.

“Kwa sasa hakuna haja ya kuwaficha watoto hao, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatoa huduma za kiuchunguzi na ile inayothibitika inatawala kati ya kiume na kike, inajengewa uwezo na kufanya kazi,”alisema

Alisema uchunguzi wa kimaabara una uwezo wa kutambua kuwa mtoto huyo ni mwanamke au ni mwanaume na jinsi ipi ambayo haitakiwi kuwepo na wataalamu wa mkemia mkuu wanawashauri madaktari kufanya upasuaji, ili kumwezesha mtoto huyo atambulike kama ni mwanaume au mwanamke.
 
Wasomi, msaada tutani; mwana baiolojia si lazima awe daktari sio?

Hakuna jinsi ya kuwaacha mpaka wakaja kuchagua wenyewe, tena baada ya balehe? Sawa, kwamba kitaalamu watathibitisha kuwa jinsi inayotawala ni x, ila kwa huku kwetu, ni bora ikajithibitisha yenyewe kuliko kupasuliwa kichwa ilhali ugonjwa uko gotini.
 
Wasomi, msaada tutani; mwana baiolojia si lazima awe daktari sio?

Hakuna jinsi ya kuwaacha mpaka wakaja kuchagua wenyewe, tena baada ya balehe? Sawa, kwamba kitaalamu watathibitisha kuwa jinsi inayotawala ni x, ila kwa huku kwetu, ni bora ikajithibitisha yenyewe kuliko kupasuliwa kichwa ilhali ugonjwa uko gotini.
Shida ni kuwa ukimuacha akakua akaja kuchagua mwenyewe akibalehe ni kwamba kama alilelewa kama wakike halafu akikua achague kuwa wa kiume huoni hapo ndipo jamii itataharuki?na unyanyapaa utaanzia hapohapo,ni bora atambuliwe mapema ili aishi na alelewe kufuatana na jinsia yake.
 
Kwa kuwa watoto wengi wanazaliwa hospitali, ingetengenezwa sheria kwamba ikitokea mtoto kazaliwa na jinsia mbili awekwe chini ya uangalizi maalumu kama ilivyo kwa watoto njiti.
Umemaliza kila kitu, wazo lako ni bora x 100 kuliko la huyo Mkurugenzi wa Huduma na Udhibiti anayesimamia uingizaji, usambazaji na matumizi ya kemikali nchini.
 
Wanawaficha vipi wakati hao wote wanazaliwa hospitalini? labda hao wanajifungulia nyumbani.So ni suala la counseling. wazalisha/wakunga wengi wakiona watoto wa namna hiyo wanaamza kushangaa wao kwamza kabla ya mzazi,kiasi mama anaona hiyo ni dalili ya mkosi vile
 
Back
Top Bottom