Serikali kununua Tani 200,000 za Mbolea kulinda Viwanda vya ndani

Serikali kununua Tani 200,000 za Mbolea kulinda Viwanda vya ndani

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kauli aliyotoa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe jana Juni 11,2025 Dodoma

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema kuwa Serikali itanunua tani 200,000(Laki mbili) za mbolea ili kuzipeleka katika maeneo ambayo matumizi ya mbolea bado ni madogo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kulinda viwanda vya ndani.

Bashe ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Juni 11, 2025, wakati akitangaza uzinduzi wa Kiwanda cha Mbolea cha Intracom Fertilizer Ltd kilichopo Nala, Dodoma. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Juni 28, 2025, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha Watanzania kuanza kutumia mbolea zinazozalishwa na viwanda vya ndani na kujionea matokeo yake katika uzalishaji wa kilimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Intracom Fertilizers Ltd, Nduwimana Nazaire, ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma na wakulima kwa ujumla kutumia mbolea zinazozalishwa na kiwanda hicho kwa kuwa zinachangia kuleta ajira nchini.

Kiwanda cha Intracom Fertilizers Ltd kinazalisha mbolea aina ya organo-mineral fertilizer — ambayo ni mchanganyiko wa mbolea ya asili (kama samadi) na mbolea za viwandani. Mbolea hiyo ina ubora wa kipekee kwa sababu inaeleza kiwango sahihi kinachotakiwa kwa kila mmea, hivyo kusaidia kuhifadhi rutuba ya udongo kwa muda mrefu.

 
Back
Top Bottom