benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema Serikali inayoongozwa na Rais
Dk. Samia Suluhu Hassan, itapeleka magari mawili ya wagonjwa na moja la kusaidia shughuli za usimamizi wa masuala ya afya katika wilaya nchini ifikapo Agosti mwaka huu.
Akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Mpwampwa, Chongolo pia alielekeza Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya' Afya, kuhakikisha vituo vya kutolewa huduma za afya vinawekewa vifaa tiba kabla ya mwisho wa mwezi Agosti mwaka huu.
"Serikali iandike kuwa hili gari ni la usimamizi na si la mkurugenzi, kwa sababu kuna tabia ya wakurugenzi kuondoka na gari la usimamizi eti anaenda katika kikao Dodoma au Morogoro huku huduma zinasimama. Mkurugenzi kama hana gari, apande basi wananchi waendelee kuwa na uhakika wa huduma.
"Tufike mahali tuone umuhimu wa kuwahudumia wananchi, hatutaona shida ya kutumia usafiri wa aina yoyote. Kama gari lako bovu gari la afya sio mbadala wake, na hivyo hivyo kwa magari ya elimu au mengine yanayopelekwa kwa shughuli maalum.