Serikali kupitia LATRA yaruhusu mabasi ya abiria kuanza safari za mikoani Saa 11 Aflajiri

Serikali kupitia LATRA yaruhusu mabasi ya abiria kuanza safari za mikoani Saa 11 Aflajiri

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,436
Reaction score
10,944
Hamjambo!

LATRA imetoa kibali cha ruhusa kwa mabasi ya Abiria wa mikoani kuanza safari kuanzia saa 11 alfajiri badala ya saa 12 kama ambavyo imezoeleka.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka LATRA, kikao cha wadau kimeafikiana uamzi huo hasa kwa Mabasi ya masafa marefu.

Kwa uamzi huu, abiria jiandae kuachwa sana na Mabasi 👇

20230116_061123.jpg
 
Uchumi ufanye kazi masaa 24, wenye mabasi watachagua, aondoke saa 11, 12.....mtu anayeenda Kagera anaweza asiwe analala kahama
 
safari ngumu ni ya kwenda Mkoa wa Kigoma haswa kutokea DSM kkwenda Kigoma wasafiri lazima walale njiani kisha asubuhi wanaanza tena safri!

hii ni kero kubwa sana kwa wasafiri, inasababisha usumbufu lakini pia inaleta hasara kwa wafanyabiashara, safari ya siku mbili!
 
safari ngumu ni ya kwenda Mkoa wa Kigoma haswa kutokea DSM kkwenda Kigoma wasafiri lazima walale njiani kisha asubuhi wanaanza tena safri !!!!

hii ni kero kubwa sana kwa wasafiri, inasababisha usumbufu lakini pia inaleta hasara kwa wafanyabiashara, safari ya siku mbili!!!
Sababu ya majambazi
 
Masoko hayajifungi, bali hufungwa na wenye biashara. Mtu anaishi Mbande anafunga usiku akimtegemea nani kuja nunua bidhaa?
Huwa yanafungwa na Sheria ndivyo zinataka ,unakuta wameweka migambo kabisa..

Ni hivi ukifunga wengine waendelee pale pale Nje ya frame yako
 
Tutalala kwenye vituo vya mabadi kama wale ndugu zetu wakuleee
 
Huwa yanafungwa na Sheria ndivyo zinataka ,unakuta wameweka migambo kabisa..

Ni hivi ukifunga wengine waendelee pale pale Nje ya frame yako
Ndani ya EA ...Rwanda, Uganda, Kenya usafiri wa umma 24/7 kigali soko wanafunga saa 6 usiku... Bank saa nne usiku kwanini uchumi usikimbie.

Sisi tunafukuzana na muda kuwahi bank ikifika saa 9:30 alasili huingii... sokoni ikifika saa 1130 jioni huingii... maduka makubwa kufunguliwa mpaka saa 3 mengine saa4 kufungwa saa 10 ujinga mzigo sana.
 
Ndani ya EA ...Rwanda, Uganda, Kenya usafiri wa umma 24/7 kigali soko wanafunga saa 6 usiku... Bank saa nne usiku kwanini uchumi usikimbie. Sisi tunafukuzana na muda kuwahi bank ikifika saa 9:30 alasili huingii... sokoni ikifika saa 1130 jioni huingii... maduka makubwa kufunguliwa mpaka saa 3 mengine saa4 kufungwa saa 10 ujinga mzigo sana.

Kama nchi tumewekewa mlolongo wa mamlaka za udhibiti zisizokuwa na tija yoyote.

Wapinzani wayaone haya na kuja na muarobaini kamili.

Hii nchi inahitaji kusukwa upya from scratch.
 
Back
Top Bottom