Serikali kupitia TAMISEMI, yawaita kazini waliotuma maombi ya Udaktari mwezi Agosti

Serikali kupitia TAMISEMI, yawaita kazini waliotuma maombi ya Udaktari mwezi Agosti

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi za ajira ya Madaktari zilizotangazwa na Serikali mwezi Agosti, 2020 kuwa zoezi la uchambuzi wa maombi yaliyopokelewa limekamilika.

Aidha, waombaji wa nafasi za ajira ya Madaktari waliokidhi vigezo wamepangiwa kazi katika Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali za Wilaya/Halmashauri nchini.

Madaktari wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

1. Kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kuanzia tarehe 23 Septemba, 2020 hadi 30 Septemba, 2020. Aidha, waombaji watakaoshindwa kuripoti kwenye vituo vya kazi kwa tarehe hizo bila ya taarifa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa haraka iwezekanavyo.

2. Kuwasilisha kwa waajiri wao (Wakurugenzi wa Halmashauri walizopangiwa) vyeti halisi (Originals Certificates) kwa ajili ya kuhakikiwa na waajiri kabla ya kupewa barua za ajira. Vyeti hivyo ni kama ifuatavyo:
(i) Cheti cha kuzaliwa;
(ii) Cheti cha Kidato cha Nne na Sita/Diploma;
(iii) Cheti cha Kuhitimu Shahada ya Udaktari;
(iv) Cheti cha Usajili wa Baraza la Madaktari Tanzania (MCT); na
(v) Uthibitisho wa Kumaliza Mazoezi kwa Vitendo (Internship).

3. Kwa Madaktari waliosoma nje ya nchi wanatakiwa kuwasilisha vyeti vya ithibati (Accreditation Certificates) kutoka NACTE/TCU.

Orodha ya Madaktari waliopangiwa vituo vya kazi katika Halmashauri mbalimbali nchini inapatikana kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz.

Limetolewa na:-
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais - TAMISEMI,
DODOMA.
22 Septemba, 2020

Kuona majina ya waliochaguliwa bofya HAPA
1600851403033.png


 

Attachments

Haya madaktari nendeni mkawajibike
 
Duuh kwahiyo hawataweza kuwachagua wabunge na madiwani huko walikojiandikisha!! Kazi kweli kweli!
 
kura zishadivertiwa tyr.
ila kichapo kipo pale pale.
maguloof
 
Back
Top Bottom