GE2025 Serikali kupitia TANROADS imeanza rasmi ujenzi wa daraja eneo la Jangwani, Dar es Salaam

GE2025 Serikali kupitia TANROADS imeanza rasmi ujenzi wa daraja eneo la Jangwani, Dar es Salaam

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeanza rasmi ujenzi wa daraja jipya la kisasa katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kudumu wa kuondoa changamoto ya mafuriko ya mara kwa mara yanayoathiri jiji hilo.

Daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 390, na linajengwa kwa viwango vya juu vya kisasa ili kuhakikisha uimara na usalama wa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Alinanuswe Kyamba, amesema tayari mkandarasi wa mradi amepokea malipo ya awali na ujenzi umeanza kwa kutengeneza barabara ya muda (diversion) itakayotumika kupitisha magari wakati wa ujenzi.

“Daraja hili ni la kimkakati, linalenga sio tu kupunguza madhara ya mafuriko bali pia kuboresha usafiri katika eneo hili muhimu. Ujenzi huu unahusisha pia njia za maingilio na barabara za magari pamoja na njia salama za waenda kwa miguu,” amesema Mhandisi Kyamba.

Ameongeza kuwa mradi huu ni sehemu ya juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Daraja la Jangwani linalotarajiwa kukamilika ndani ya muda uliopangwa, litachangia kuimarisha mfumo wa usafiri kati ya katikati ya jiji na maeneo ya Ilala, Buguruni, pamoja na sehemu nyingine zinazotegemea barabara ya Morogoro.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa mradi huu na kuuwezesha kuanza. Wananchi wamekuwa wakingoja kwa muda mrefu kuona suluhisho la kudumu kwa tatizo la mafuriko ambalo limekuwa likisumbua kwa miaka mingi,” aliongeza Kyamba.

Mradi huu ni sehemu ya miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa TANROADS, ikiwemo uboreshaji wa barabara kuu na madaraja muhimu kwa maendeleo ya jiji.

523360727_18065978243236473_7566993458851788368_n.jpeg

​
 
Dr Samia Suluh Hassan hongera sana 5 tena but tutatiki bila shida endapo utalipa fidia stahiki za ardhi mapema kwa watu waliokua na offer na hati pia. Ambao hawajalipwa na malalamiko yao yapo PO-RALG hayajapata utatuzi wa haraka mpaka leo.

Mama tutatiki asubuhi na mapema ukiweza kuzingatia haki za wadai niliotaja hapo juu. Tafadhali ingilia kati watu walipwe mapema tubaki na kazi ya kutiki tu
 
Huo ujenzi uko wapi? Mbona umetuwekea picha ya morogoro road!
 
Mama anaupiga mwingi. Mitano tena
Anna Tibaijuka alishasema wazi jinsi mabosi wake walivyoshupaza shingo alipokataa kile kituo kujengwa pale. Sijui wanasiasa huwa wanajisikiaje kutia hasara hela za walipa kodi kiasi hiki.
 
Kwa kweli jiji likiwa na Mto au Mito hupendeza sana ila sisi sijui tunakosea wapi.

Kuna majiji duniani walitamani kuwa na Mito basi wakaamua kuwa na man made
Yaani wahandisi Wetu wanajua barabara tu
 
Dr Samia Suluh Hassan hongera sana 5 tena but tutatiki bila shida endapo utalipa fidia stahiki za ardhi mapema kwa watu waliokua na offer na hati pia. Ambao hawajalipwa na malalamiko yao yapo PO-RALG hayajapata utatuzi wa haraka mpaka leo.

Mama tutatiki asubuhi na mapema ukiweza kuzingatia haki za wadai niliotaja hapo juu. Tafadhali ingilia kati watu walipwe mapema tubaki na kazi ya kutiki tu
Mhanga mwenzangu tuliobakia wa mradi wa bonde la mto msimbazi,nimektumia meseji namba yangu tuweze kuzungumza ama kupeana taarifa mbalimbali zinazojiri
 
Mhanga mwenzangu tuliobakia wa mradi wa bonde la mto msimbazi,nimektumia meseji namba yangu tuweze kuzungumza ama kupeana taarifa mbalimbali zinazojiri
Nimekutext wapo mbioni kulipa. Isipokuwa kuna kuna kitengo kinaitwa SC cimmmitee kimelala sana hakijui kwamba wanakwamisha nia njema ya raisi. Watu walipwe October tutiki kwa wino mzito. Wasipolipa hatutiki
 
Ila mie nionavyo itafikia iyo Oktoba na wasilipe kulipa itakuwa labda mpaka uchaguzi upite
 
Ila mie nionavyo itafikia iyo Oktoba na wasilipe kulipa itakuwa labda mpaka uchaguzi upite
Wao watu wa PO RALG ndio wametoa taarifa kwa mfadhili wao World Bank kwamba SC committee iki approval mapendekezo basi ndani ya August na September huenda watu wakalipwa
Sasa hao SC committee ndio wanaochelewesha mambo. Sasa mh Raisi akiwaona hao wazembe wanamuharibia kwa kuchelewesha mambo watu wasilipwe kwa wakati inabidi awatimue haraka.
ili October tutuki vizuri tukiwa tumeshalipwa fidia zetu vizuri
 
Back
Top Bottom