Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekabidhi jumla ya Sh bilioni 2 kwa wanufaika wa shughuli za utalii na uhifadhi wa wanyamapori, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi zinazotokana na rasilimali za utalii. Fedha hizo zinatarajiwa kuchochea shughuli za maendeleo katika maeneo yanayozunguka hifadhi na kuimarisha ushirikiano kati ya jamii na uhifadhi.