Serikali kupunguza kodi kwenye betting haioni inaendelea kuharibu vijana ambao wapo addicted na kubet

Serikali kupunguza kodi kwenye betting haioni inaendelea kuharibu vijana ambao wapo addicted na kubet

Protector

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Posts
422
Reaction score
893
Leo waziri wa fedha amependekeza kupunguza kodi kwenye pesa anayoshinda mtu aliyebeti kutoka 15% mpaka 10%.

Kwangu naona hii ni kama kuendelea kuharibu vijana maana watahamasika kutokana na kuona wakishinda watakatwa pesa kidogo.

Bora ingeongezwa ili iwavunje moyo watu wanaobet labda wangetafuta shughuli zingine.
 
Ndiyo sekta iliyoajiri vijana wengi sikuizi, kama huko serikalini wameongezewa mishahara bas na hawa wa betting nao wanaongezewa kidogo. Na mheshimiwa waziri ni mzee wa kubet pia
 
Tunacholiwa NI kingi KULIKO tunachokula.
Kampuni za betting ndo zinatakiwa zitulipie Kodi maana sio kwa vipigo hivi
 
Serikali inapata hela nyingi unaposhindwa kuliko unavyoshinda, Wana hesabu zao.
 
Kazi yoyote ambayo haizalishi huduma wala bidhaa inayosaidia jamii husika, ni kazi ya kishaitwani tu. Ni kazi feki.

Furaha yoyote unayoipata bila kupitia kuwafurahisha wanajamii fulani, labda umewalisha, umewaburudisha, umewatibu, umewafundisha, umewasogezea bidhaa [biashara], umewaongoza kwenye maendeleo etc............ furaha zisizo na elementi yoyote ya watu ni furaha feki.

Kazi yoyote ambayo haina uhusiano wa moja kwa moja [direct proportionality] kati ya juhudi na matokeo haiwezi kumpa mtu utoshelevu ile satisfication ya ndani.

Pamoja na mengine mengi yanafanya kubeti kusiwe jambo la kushadadia kama kazi rasmi.

Kubeti kubakie tu kama mchezo wa kujifurahisha hapo sina pingamizi. Kama betting ndo tunategemea itukwamue tunajidanganya ---- Focus iwe kwenye uzalishaji bidhaa na huduma/product and services
 
Back
Top Bottom